Glosofobia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Glosofobia (kwa Kiingereza: glossophoby) ni hofu au dukuduku la kuzungumza hadharani. [1]

Neno glosofobia linatokana na maneno ya Kigiriki γλῶσσα glōssa, likimaanisha ulimi na φόβος phobos, hofu.

Kitendo cha kuongea hadharani, iwe ni mbele ya kundi la watu wasiojulikana au mbele ya kundi la marafiki, ndio sababu inayompa wasiwasi mzungumzaji. Mzungumzaji anaweza kuongea bila matatizo mbele ya kundi la watu asiowajua, lakini akashindwa kuongea mbele ya marafiki au familia na kinyume chake. Baadhi huongea bila matatizo mbele ya kundi dogo na wengine hufanya hivyo mbele ya kundi kubwa.[2]

Utafiti[hariri | hariri chanzo]

Utafiti uliofanywa kwenye Chuo Kikuu cha Tennessee Knoxville unaonyesha hali hii hutokana na wasiwawasi na hofu na hisia ya kutotulia.[3]

Inakadiriwa kuwa alimia 75 ya watu wote huwa na kiwango fulani cha wasiwasi wanapozungumza hadharani.[4] Hali hii isipopatiwa suluhisho huweza kudhuru ubora wa maisha, malengo ya ajira na maeneo mengine. Kwa mfano, malengo ya kielimu yanayohitaji kuzungumza hadharani yanaweza yasifikiwe. Hata hivyo, si wale wote wenye tatizo hili wanashindwa kukamilisha malengo ya ajira.

Utafiti uliofanywa na Garcia-Lopez, Diez-Bedmar na Almansa-Moreno umeonyesha kuwa wanafunzi waliowahi kufunzwa jinsi ya kuzungumza hadharani wanaweza kuwa walimu wa wanafunzi wengine kuwasaidia kuimarisha uwezo wao wa kuongea hadharani.[5]

Kama Garcia-Lopez (2013)[6] alivyotambua, dalili zake zinajumuisha kuongezeka kwa mapigo ya moyo, kukauka kwa mdomo, kupanuka kwa mboni za jicho, kutoka jasho, kutetemeka n.k. Dalili hizo huweza kuzuiliwa au kupungunzwa kwa kutumia dawa.

Msaada na tulizo[hariri | hariri chanzo]

Kozi za kuzungumza hadharani au mashirika kama vile Australian Rostrum, Toastmasters International, POWERtalk International, na Association of Speakers Clubs huweza kusaidia watu kupunguza wasiwasi. Baadhi ya watu hutumia dawa kama vile beta blocker.

Wakati mwingine, wasiwasi huweza kupunguzwa kama mzungumzaji atajitahidi kutopambana na wasiwasi wake.[7] Mzungumzaji anaweza kupunguza wasiwasi pia kama anafahamu vyema mada anayozungumzia. Inashauriwa pia mzungumzaji afanye mazoezi ya kuongea mbele ya kundi dogo la watu. Zaidi ya hiyo, mzungumzaji anaweza kuzungumza huku akiwatazama watu wanaosikiliza kwa makini na kiurafiki.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Fritscher, Lisa. "Glossophobia". About.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-28. Iliwekwa mnamo 13 March 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. sergy, Lauren. "Handy Answer: The Handy Commnnication Answer Book". Florida Academic Library Services Cooperative. Visible INK Press. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-05-25. Iliwekwa mnamo 13 October 2018.  Check date values in: |accessdate= (help)
  3. "School of Communication Studies". School of Communication Studies The University of Tennessee Knoxville. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-06-05. Iliwekwa mnamo 5 December 2018.  Check date values in: |accessdate= (help)
  4. Hamilton, C. (2008) [2005]. Communicating for Results, a Guide for Business and the Professions (eighth edition). Belmont, CA: Thomson Wadsworth. 
  5. Garcia-Lopez, L. J.; Diez-Bedmar, M.B. & Almansa-Moreno, J.M. (2013). "From being a trainee to being a trainer: helping peers improve their public speaking skills". Journal of Psychodidactics 18 (2): 331–342. doi:10.1387/RevPsicodidact.6419. 
  6. Garcia-Lopez, L.J. (2013). Treating...social anxiety disorder. Madrid: Piramide. 
  7. Grice, George L. (2015). Mastering Public Speaking 9th Edition. Pearson. uk. 29. ISBN 0133753832. 

Bibliografia[hariri | hariri chanzo]

  • Rothwell, J. Dan. In The Company of Others: An Introduction to Communication. New York: McGraw Hill, 2004.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]


Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Glosofobia kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.