Nenda kwa yaliyomo

Germaine Kamayirese

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Germaine Kamayirese, ni mhandisi na mwanasiasa nchini Rwanda, ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Usimamizi wa Dharura na Masuala ya Wakimbizi kwenye baraza la mawaziri la Rwanda, kuanzia tarehe 18 Oktoba 2018 [1] hadi alipoondolewa kwenye baraza la mawaziri tarehe 27 Februari 2020.

Kabla ya hapo, kuanzia tarehe 24 Julai 2014 hadi tarehe 18 Oktoba 2018, alihudumu kama Waziri wa Nchi wa Miundombinu anayehusika na Nishati, Maji na Usafi wa Mazingira. [2] [3]

Historia na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa Wilaya ya Nyarugenge tarehe 5 Agosti 1981. Kuanzia mwaka 2000 hadi 2005, alisoma katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Kigali (KIST), ambayo leo ni Chuo cha Sayansi na Teknolojia (Rwanda), chuo kikuu cha Rwanda . Ana Shahada uzamili ya Uhandisi wa Umeme, iliyotolewa na KIST mnamo mwaka 2005. Pia ana Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Mawasiliano, aiyotunukiwa kwa pamoja mwaka 2010 na KIST na Chuo Kikuu cha Coventry, nchini Uingereza. [4] [5]

Kuanzia mwaka 2008 hadi 2011, Germaine Kamayirese aliwahi kuwa mtaalamu wa mtandao kwenye kampuni ya "Rwanda Utilities Regulatory Agency" (RURA). Kuanzia mwaka 2012 hadi 2014, alihudumu kama mtaalamu wa mtandao kampuni ya "Tigo-Rwanda". [6] Kuanzia mwaka 2010 hadi 2011 Kamayirese alihudumu kama mshauri kwenye taasisi ya "Institute of Engineering Architecture Rwanda". Kufikia Septemba 2017, alikuwa mwanachama wa "Rwanda Women Engineers Association" (RWEA). [7]

Germaine Kamayirese ni mama wa watoto wanne. [8]

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
  1. Jean de la Croix Tabaro (18 Oktoba 2018). "Rwanda Gets New 50-50 Gender Cabinet, Fewer Ministers". KTPress. Iliwekwa mnamo 19 Oktoba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Umutesi, Doreen (31 Julai 2014). "Meet the new female faces in cabinet". Iliwekwa mnamo 17 Septemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Minifra (24 Julai 2014). "Germaine Kamayirese: The Minister of State in Charge of Energy, Water and Sanitation's Biography". Rwanda Ministry of Infrastructure (Minifra). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Septemba 2018. Iliwekwa mnamo 17 Septemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Umutesi, Doreen (31 Julai 2014). "Meet the new female faces in cabinet". Iliwekwa mnamo 17 Septemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)Umutesi, Doreen (31 July 2014). "Meet the new female faces in cabinet". New Times (Rwanda). Kigali. Retrieved
  5. Minifra (24 Julai 2014). "Germaine Kamayirese: The Minister of State in Charge of Energy, Water and Sanitation's Biography". Rwanda Ministry of Infrastructure (Minifra). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Septemba 2018. Iliwekwa mnamo 17 Septemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)Minifra (24 July 2014). "Germaine Kamayirese: The Minister of State in Charge of Energy, Water and Sanitation's Biography". Kigali: Rwanda Ministry of Infrastructure (Minifra). Archived from the original on 16 September 2018. Retrieved
  6. Minifra (24 Julai 2014). "Germaine Kamayirese: The Minister of State in Charge of Energy, Water and Sanitation's Biography". Rwanda Ministry of Infrastructure (Minifra). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Septemba 2018. Iliwekwa mnamo 17 Septemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)Minifra (24 July 2014). "Germaine Kamayirese: The Minister of State in Charge of Energy, Water and Sanitation's Biography". Kigali: Rwanda Ministry of Infrastructure (Minifra). Archived from the original on 16 September 2018. Retrieved 17 September
  7. Umutesi, Doreen (31 Julai 2014). "Meet the new female faces in cabinet". Iliwekwa mnamo 17 Septemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)Umutesi, Doreen (31 July 2014). "Meet the new female faces in cabinet". New Times (Rwanda). Kigali>. Retrieved
  8. Umutesi, Doreen (31 Julai 2014). "Meet the new female faces in cabinet". Iliwekwa mnamo 17 Septemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)Umutesi, Doreen (31 July 2014). "Meet the new female faces in cabinet". New Times (Rwanda). Kigali. Retrieved
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Germaine Kamayirese kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.