George Kinyonga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

George Peter Kinyonga (alizaliwa nchini Tanzania, Desemba 24, 1992) alikuwa mwanamuziki mashuhuri nchini Kenya.

Peter Kinyonga na kaka yake aitwaye Wilson Kinyonga ndio waanzilishi wa bendi ya rumba Simba Wanyika [1]ambayo baadaye ikazaa bendi kama Les Wanyika, Super Wanyika Stars na nyingine.

George na Wilson Kinyonga walianza muziki katika mji wao wa nyumbani Tanga nchini Tanzania, ambapo ndipo walipojiunga kwenye bendi ya Jamhuri Jazz mwaka 1966. Wao walihamia Arusha mwaka 1970 na wakaanzisha bendi ya Arusha Jazz pamoja na kaka yao William Kinyonga. Mwaka 1970 walihamia nchini Kenya na kuanzisha Simba Wanyika, ambayo ikaja kuwa moja kati ya bendi mashuhuri kwenye historia ya muziki wa Afrika Mashariki.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Simba Wanyika: Afropop Band -- Kenya, East Africa". web.archive.org. 2006-05-02. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-05-02. Iliwekwa mnamo 2023-02-26. 

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu George Kinyonga kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.