Nenda kwa yaliyomo

Les Wanyika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Les Wanyika ilikuwa bendi maarufu nchini Kenya na Tanzania na wanachama wake walikuwa wakiishi nchini Kenya. Ilianzishwa mwaka wa 1978 na mpiga gitaa Omar Shabani, mpaza sauti Tom Malanga na wanachama wengine wa bendi ya Simba Wanyika. John Ngereza na Issa Juma walijiunga nao baadaye.

Les Wanyika waliimba nyimbo nyingi maarufu, lakini walikumbukwa sana kwa nyimbo zao za mwaka wa 1979 Sina Makosa na Paulina. Issa Juma aliihama bendi hiyo baadaye ili kuendeleza shughuli zake nyingine za kimuziki. Kundi hilo liliendelea mpaka Omar Shabani alipofariki mwaka wa 1998. John Ngereza alifariki miaka miwili baadaye.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mwaka wa 1971, ndugu wawili kutoka pwani ya mkoa wa Tanga, Tanzania, Wilson Kinyonga na George walianzisha bendi waliyoiita Simba Wanyika, kwa Kiingereza Savannah Lions. Kutokana na hali ngumu ya kiuchumi nchini Tanzania katika miaka za 1970 ambayo, wengi wa wasanii wa muziki wakati huo walihamia Kenya na nchi nyingine jirani katika hali ya kutafuta majani mabichi. Si ajabu kwamba baadhi ya wasanii hao walichukua uraia wa nchi hizo.

Wakati huo, usafiri kati ya nchi hizo mbili ulirahisishwa na kuweko kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, na mkataba wa maelewano miongoni mwa Kenya, Uganda na Tanzania. Baada ya kusambaratika kwa jamuia hiyo mwaka wa 1977, kuvuka mpakani kulikuwa na ugumu, hivyo uanzishwaji wa makao ya kudumu nchini Kenya na kundi hili. Bendi hiyo ilipoendelea na kukua, bendi kadhaa zilijitoa, lakini mashuhuri ilikuwa ni Les Wanyika.

Ni jambo moja kwa msanii kuhamia nchi nyingine katika kutafuta lisho bora na lingine kabisa kwa nchi kutoa madai ya uongo ya kumiliki baadhi ya wasanii ambao ni wahamiaji wa nchi nyingine kwa lengo la kujionyesha na kujitakia umaarufu. Hiyo inaweza kusemwa kutokana na wimbo wa Malaika ambao asili yake ni mchora vibonzo wa nchi ya Tanzania, Geofrey "Gado" Mwampembwa ambaye ni Mtanzania anayefanya kazi katika gazeti la Nation nchini Kenya na eneo la jumla la mlima Kilimanjaro. Wakenya wamekuwa vizuri sana katika taaluma hii.

Katika bendi ya Les Wanyika, wanachama wa kikundi walijumuisha pamoja Watanzania na Wakenya. Wanachama maarufu John Ngereza, Issa Juma na Omar Shabani walikuwa wote kutoka Tanzania, na Tom Malanga kutoka Kenya. Bendi hii ilikuwa na makao ya kudumu mjini Nairobi, walikotumbuiza katika vilabu vya starehe na mahoteli mbalimbali. Wengi wa wanachama wa kundi hili aidha walikufa au wameathirika na ukongwe.

Mwaka wa 2006, lilianzishwa upya na watu wengine.

Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Les Wanyika kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.