Simba Wanyika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Simba Wanyika ilikuwa bendi nchini Kenya iliyoundwa mwaka wa 1971 na mandugu kutoka Tanzanian Wilson Kinyonga na George Kinyonga, na ilitupiliwa mbali mwaka wa 1994. Simba Wanyika , na bendi zingine mbili zilizodondoka kutoka kwayo Les Wanyika na Super Wanyika Stars, zilikuwa bendi mashuhuri sana nchini Kenya. Muziki wao uliotokana na sauti ya gitaa, ikiongozaw na mpiga gitaa wa Soukous, Dr Nico,ikichanganywa na maneno matamu ya muziki wa rumba na kuimbwa katika Kiswahili. Simba wa nyika maana yake "Lions of the Savannah" katika Kizungu.

Wilson Kinyonga na George Kinyonga walianza muziki katika mji wao wa nyumbani wa Tanga nchini Tanzania walipo jiunga na Jamhuri Jazz Band mwaka wa 1966. Walihamia Arusha mwaka wa 1970 na kuunda bendi ya Arusha Jazz na ndugu yao mwingine, William Kinyonga. Katika kipindi hiki, wanamuziki wangeweza kusafiri watakavyo kati ya Kenya na Tanzania, na muziki wa Kenya ukashawishika sana na wanamuziki wa rumba wa Tanzania. Mwaka wa 1971 mandugu hawa wa Kinyonga walihamia nchini Kenya na kuanzisha Simba Wanyika. Bendi ilitumbuiza katika vilabu vya usik na mabaa katika jijini Nairobi, nakupata wafuasi wengi mno, na katikati ya miaka ya 1970, walikuwa wanajulikana kote Kenya, kwa ajili ya magoma kama "Mwongele" na "Wana Wanyika". Walikuwa bendi bora kuliko bendi nyingine za rumba na hakuna bendi ingepambana nao nchini Kenya kutokana na kufungwa kwa mpaka wa Tanzania mwaka wa 1975.

Kutekelezwa kwa vikwazo baina ya mpaka wa Kenya-Tanzania ilisababisha watu kukua kwa muziki na kuelekea katika mtindo wa uliokuwa unajitokeza wa benga nchini Kenya Simba Wanyika waliendelea kucheza rumba, na walikuwa bado maarufu wakti bendi ilipogawanyika katika miaka ya 1970 wakati mpiga gitaa Omar Shabini alichukua wengi wa wanamuziki na kutengeneza Les Wanyika. Mwaka wa 1980, George Kinyonga pia alijiondoa katika Simba Wanyika, akichukua wanamuziki zaidi pamoja naye na kuunda bendi ya Orchestra Jobiso. Lakini baadaye alirudia Simba Wanyika huku bado akifanya miradi za upande na Jobiso. Simba Wanyika baadaye walibadilisha jina lao hadi "Simba Wanyika Original" ili kuzuia mkanganyiko na Les Wanyika na kundi lilotoweka kutoka kwayo la, Super Wanyika Stars.

Simba Wanyika ilirudia umaarufu wake katika katikati ya miaka ya 1980 , wakitoa magoma mengine motomoto na kuzuru Ulaya mwaka wa 1989. Bendi ilitupiliwa mbali mwaka wa 1994, lakini bendi kadhaa zilizotokana nayo bado zinaendelea kucheza.

Angalia Pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]