Odi Pop

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Gengetone)
Jump to navigation Jump to search

Odi Pop au Gengeton ni mtindo wa muziki maarufu nchini Kenya ambao unatokana na aina mbalimbali za muziki kama Genge, Hip Hop na Reggaeton na kuchanganya ushawishi kutoka kwa muziki wa Reggae na Dancehall, na kujenga kwenye msingi wa mahadi ya Kiafrika.

Unaimbwa kwa njia ya kufoka kwa lugha ya Kiswahili pamoja na ya Sheng. [1] Kuna tanzu kadhaa kutoka kwa tanzu hii (inayojulikana kwa jina la jumla Odi pop) kama vile: Dabonge, Debe na nyinginezo. Muziki huo unaongozwa na vijana wa Kenya na wengi wao wanaandika muziki kama bendi.

Neno Odi Pop lilibuniwa mnamo 2019 na msomi wa mziki na mwanamuziki Dan 'chizi' Aceda, ambaye ni maarufu kwa muziki wa Benga. Alielezea alivyo fikia neno hilo kwenye chapisho la The Elephant:

Kwa sababu ya utaratibu wa majina, ninapendekeza neno la pamoja "Odi-pop" kurejelea mitindo yote ya sanaa hii mpya. Ninajua kila kundi lina jina lao la kando kando mfano; Gengetone, mtindo wa Dabonge na kadhalika na ufafanuzi wangu sio kujaribu kufuta hayo. Kwangu huu mtindo wa mziki kimsingi ni pop lakini na sauti ya pamoja (inayotumia mvuto wa hip-hop pamoja na kuchanganya miradi ya mashairi ya Karibiani na yote yamejengwa kwa msingi wa mtungo wa Kiafrika na kuimbwa kwa marudio ya rap na viunzi vya Kiswahili na Sheng). Utaratibu wangu wa kutaja umekopa kutoka K-Pop. [2]

Wasanii kama Ethic wamekemea jina Odi pop na wanapendelea istilahi gengeton (wakati mwingine inaandikwa Gengetone ) . Neno Gengeton lina kopa kutoka tanzu mbili za mziki ambazo ni; Genge, utanzu ambao ilikuwa maarufu nchini Kenya katika miaka ya 2000 na utanzu wa Reggaeton. [3]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Asili[hariri | hariri chanzo]

Daddy Owen at the Groove Awards
Daddy Owen kwenye sherehe ya Groove Awards.

Mizizi ya mapema ya Odi pop inaweza kupatikana toka mziki wa Injili wa miaka ya 2000' ambao ulikiuka tamaduni za kanisa ya wakati huo. [4] Mziki wakati huo uliendeshwa sana na "ujumbe" na "maana" ambayo ilisababisha uchu ya muziki wa dansi. Wanamuziki maarufu Rufftone na ndugu yake Daddy Owen wanasifiwa kuwa wavumbuzi wa mwanzo katika muziki wa pop wa Kikristo. Mziki wao uliondoka kwenye tamaduni za wakati huo na kuleta enzi mpya ya mziki wa Kikristu ambao ulikuwa na dansi zaidi na ulihusiana zaidi na vijana.

Miaka ya 1990 na 2000, serikali ya Kenya pamoja na kanisa walikuwa na udhibiti mkubwa kwa ya yaliyorushwa hewani kwani kulikuwa na mtangazaji mmoja tu. [5] Serikali iliwadhulumu wasanii kadhaa ambao walishtakiwa kama maadui wa nchi. Jambo hili lili sababisha kuongezeka kwa umaarufu wa mziki wa injili. [6]

Mnamo 2002, Gidi Gidi Maji Maji waliachilia 'Unbwogable' ambayo ilitumika kama wimbo rasmi wa kampeni ya mgombea Rais Mwai Kibaki, na mgombea mwenza Waziri Mkuu wa pili nchi ya Kenya, Raila Odinga katika uchaguzi wa mwaka ishirini na mbili, 2002. Lebo ya mziki Ogopa DeeJays ilikuwa maarufu katika kipindi hiki pia. Wamekuza talanta za wanamuziki wengi mashuhuri kama vile E-Sir, K- Rupt, Nameless, Amani, na wengineo. Ogopa Deejays ni lebo mojayapo yenye ushawishi mkubwa nchini Kenya na tanzu yao inaitwa Boomba Music (pia inajulikana kama Kapuka). Boomba ni moja wapo ya misingi ya Odi Pop.

Katika kipindi hicho pia, aina ya mziki inayoitwa Genge ilikuwa inapaa ikiongozwa na wasanii maarufu Jua Cali na Nonini kutoka Calif Records . Jina Genge lilitokana na mtayarishaji wao wa mziki Clemo . [7] [8] Jarida The Poetics of Genge: Jua Cali's Niimbe iliwasilishwa katika mkutano wa MELUS wa ishirini na sita wa kila mwaka,na katika mkutano wa sita wa Jumuiya ya Amerika ya Fasihi na masomo ya Lugha (USACLALS), Chuo Kikuu cha Santa Clara, California . [9] Katika miaka iliyofuata wasanii kama Mejja, Madtraxx, Jimwat na wengineo walichangia kufuka kwa tanzu ya Genge. [10] [11]

Mnamo Oktoba 2016, mwanamziki Collo kutoka kikundi Kleptomaniax aliachilia kibao 'Bazokizo' akishirikiana na Bruz Newton, wimbo ambao ulishinikiza hatima ya Odi Pop. [12] Odi pop ililetwa kwa macho ya uma baada ya Bazokizo kupeperushwa kwenye televisheni na redio mara nyingi. Hii ilifungua milango kwa wanamuziki wengine wa Odi pop wakiwemo Timeless Noel na Jabidii. [13] Mtindo huu umeibuka kutoka eneo la Nairobi haswa katika mkoa wa Eastlands ikijumuisha Kayole, Dandora, Umoja, Dagoretti, na Rongai.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Aceda (2019-09-12). DAN ACEDA - How Kenyan Gospel Pop Birthed the Odi-Pop Craze | The Elephant (en-US). Iliwekwa mnamo 2019-09-14.
 2. Aceda (2019-09-12). DAN ACEDA - How Kenyan Gospel Pop Birthed the Odi-Pop Craze | The Elephant (en-US). Iliwekwa mnamo 2019-09-14.
 3. Genge Music | African Music Genres (en-US). Iliwekwa mnamo 2019-09-14.
 4. Aceda (2019-09-12). DAN ACEDA - How Kenyan Gospel Pop Birthed the Odi-Pop Craze | The Elephant (en-US). Iliwekwa mnamo 2019-09-14.
 5. "Kenya Special Musical History". 
 6. The politics of music in Africa (en). Daily Nation. Iliwekwa mnamo 2019-09-14.
 7. Genge Music | African Music Genres (en-US). Iliwekwa mnamo 2019-09-14.
 8. Adol. When Kapuka and Genge gave Kenyan music true identity (en). UREPORT-CITIZEN JOURNALISM. Iliwekwa mnamo 2019-09-14.
 9. Wanjala (2012). The Poetics of Genge: Jua Cali's Niimbie. A paper presented at the 26th annual MELUS conference and 6th conference of the United States Association for Commonwealth Literature and Language Studies (USACLALS), University of Santa Clara, California, United. profiles.uonbi.ac.ke. Iliwekwa mnamo 2019-09-14.
 10. PHOTO - When Mejja First Came to Nairobi in 2007 (en-US). Nairobi Wire (2015-02-20). Iliwekwa mnamo 2019-09-14.
 11. Artist of the day: Mejja aka Okonkwo - News | Mdundo.com (en). mdundo.com. Iliwekwa mnamo 2019-09-14.
 12. Nzyoka (2019-07-08). Odi pop is here to stay just ask Koroga (en-US). KBC | Kenya's Watching. Iliwekwa mnamo 2019-09-14.
 13. ONE ON ONE: Timeless Noel (en). Daily Nation. Iliwekwa mnamo 2019-09-14.
Musical notes.svg Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Odi Pop kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.