Nenda kwa yaliyomo

Fungo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fungo
Fungo (Civettictis civetta)
Fungo (Civettictis civetta)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Carnivora (Wanyama mbua)
Nusuoda: Feliformia (Wanyama kama paka)
Familia: Viverridae (Wanyama walio na mnasaba na paka-zabadi)
Nusufamilia: Viverrinae (Wanyama wanaofanana na paka-zabadi)
J.E. Gray, 1821
Jenasi: Civettictis
Pocock, 1915
Spishi: C. civetta
(Schreber, 1776)
Msambao wa fungo
Msambao wa fungo

Fungo, fungo wa Afrika, ngawa au paka-zabadi wa Afrika (Civettictis civetta) ni mnyama mbua na spishi pekee ya jenasi yake[1]. Pia ni mwanafamilia mkubwa kabisa wa Viverridae. Binturongi ni mfupi lakini mzito kuliko fungo. Spishi hii inatokea mahali pengi pa Afrika kusini kwa Sahara. Hukiakia usiku hasa na kulala mchana katika uoto mzito. Usiku huonekana katika maeneo mbalimbali kutoka msitu mzito hadi mbuga.

Fungo ni mamalia wapweke wenye rangi nyeusi na nyeupe kwa milia na mabaka. Kwa hivyo wanyama hawa ni ngumu kuona vizuri kwa mwanga mhafifu. Wanaweza kutofautishwa pia kwa matako yao makubwa na manyoya ya mgongo yanayoweza kuwekwa wima. Hula vitu vyingi kama wanyama wadogo, wadudu, mayai, mizoga na mimea. Wanaweza kula wadudu na wanyama wenye sumu, kama tandu, majongoo na nyoka. Hugundua mawindo yao kwa harufu na sauti badala ya kuona.

Kama wanyama wengine wa familia yao fungo watoa kioevu kiitwacho civetone au zabadi. Kioevu hiki kipakazwa juu ya miti, mawe n.k. ili kudai eneo lao. Zabadi hutumika katika viwanda vya manukato pia na inavunwa kutoka fungo wafugwao k.m. huko Uhabeshi.

  1. Ray, Justina C. "Mammalian Species: Civettictis civetta." The American Society of Mammalogists (1995): 1-7. Print.