Nenda kwa yaliyomo

Frida Kahlo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Frida Kahlo & Diego Rivera (1932)

Magdalena Carmen Frida Kahlo y Calderón (6 Julai 190713 Julai 1954) alikuwa mchoraji nchini Mexiko. Amejulikana kwa picha zake zinazotumia rangi zenye nguvu na maumbo ya sanaa ya kienyeji ya Mexiko.

Frieda alizaliwa na baba Mjerumani aliyehamia Mexiko na mama mwenye asili ya Kiindio. Alipokuwa na miaka 18 alipatwa na ajali nzito ya basi akaendelea kuishi kwa maumivu kila siku, na hakuweza kuzaa watoto. Aliolewa na mchoraji Diego Rivera, alifanya kazi pamoja naye hata kama huyu hakuwa mwaminifu kwake mara kwa mara.

Picha nyingi zinaonyesha maumivu yake yeye mwenyewe na hali ngumu ya wakina mama. Nyumba alimoishi kati ya miaka 1929-1954 imekuwa makumbusho yake.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Frida Kahlo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.