Fly Me to the Moon
"Fly Me to the Moon" | ||
---|---|---|
Wimbo wa Frank Sinatra
kutoka katika albamu ya It Might as Well Be Swing | ||
Umetolewa | 1964 | |
Umerekodiwa | 9 Juni 1964 | |
Urefu | 2:30 | |
Studio | Reprise Records | |
Mtunzi | Bart Howard | |
Mtayarishaji | Sonny Burke |
"Fly Me to the Moon" ni wimbo wenye miondoko ya pop uliotungwa na kuandikwa na Bart Howard mwaka 1954. Ulipewa jina la asili la n Other Words na ulipelekwa kwa mara ya kwanza katika utambuzi wa nyimbo na Felicia Sanders. Wimbo huu ukaja kujulikana na kupata umaarufu baadae na kujulikana kama Fly Me to the Moon tangu uetngenezwe, na miaka michache baadae watunzi wa wimbo huu waliamua kubadilisha jina la wimbo huo rasmi na ukawa unajulikana kama 'Fly Me to the Moon'
Historia
[hariri | hariri chanzo]Wimbo huu ulirekodiwa kwa mara ya kwanza mwaka 1954, na Kaye Ballard na kuuzwa na Decca Records kama kijisehemu cha single kilichokuwa na namba 29114. Mnamo mwaka 1956, wimbo huu ulirekodiwa kwa mara ya pili na Portia Nelson katika albamu yake ya ‘Let Me Love You’ na katika mwaka huo huo, mwanamuziki mwingine aliyejulikana kama Johnny Mathis alirekodi wimbo huom kwa mara nyingine tena, hii ikawa ni mara ya kwanza kwa jina la ‘’Fly Me to the Moon’’ kutokezea katika kava la juu la rekodi hiyo
Mwimbaji halisi wa wimbo wa Fly Me to the Moon Felicia Sanders alirekodi wimbo huu mwaka 1959, na kutayarishwa na Studio ya Decca Recoeds na kutoka na hati namba 30937
Katika siku za mwisho za mwaka 1961, mwanamuziki mwingine Nat King Cole alirekodi wimbo huo katika albamu yake ya ‘’Nat King Cole Sings/ Shearing Plays’’ na wimbo huo ulitoka kupitia studio za Capitol Records kwa namba ya usajili 1675
Mwaka 1962, wimbo huu ulipigwa kwa kutumia vyombo peke yake, na ulirekodiwa kama Fly Me to the Moon na ndash; Bossa Nova na mwanamuziki Joe Haenell na kuweza kufanya vizuri katika chati ya muziki ya the U.S. pop singles charts. Kwa kufanikiwa kufika hadi nafasi wa 14.
Mwimbaji wa muziki aina ya Jazz akipigiwa ngoma na Roy Haynes, na kuwashirikisha Roland Kirk, Tommy Flanagan akipiga piano na Henry Grimes akifanya bass walirekodi wimbo huo katika mahadhi yanayojulikana kama a brisk instrumental waltz for Haynes katika albamu iliyoitwa ' Out of the Afternoon katika studia za (Impulse! Records AS-23), na kufanikiwa kuutoa tarehe 16 Mei 1962.
Ukiwa katika hali yake ya asili au ya mwanzo, ukiwa umepangwa na Ernie Freeman wimbo huu unapatikana katika albamu ya Julie London ya mwaka 1963. iliyoitwa The End of the Road lakini ikiwa na mabadiliko kidogo sana hasa katika mwanzo wa wimbo huu.
Mwimbaji mwingine aliyeitwa Frank Sinatra alirudia tena kurekodi wimbo huu katika albamu yake ya mwaka 1964, iliyoitwa It Might as Well Be Swing akimshirikisha Count Basie.
Mwaka uliofuatia, mwanamuziki mwingine Tony Bennett alirekodi wimbo huo tena lakini haukuweza kufanya vizuri. Tangu miaka hiyo, hadi kufikia mwaka 2000 amekuwa akiimba wimbo huo katika matamasha mbalimbali bila kutumia kifaa cha muziki cha aina yoyte.
Oscar Peterson alirekodi wimbo huo katika albamu yake ya Tristeza on Piano mwaka 1970.Lakini wimbo huu ulifutwa kutoka katika mjumuishi wa nyimbo tatu, au kutokana na kukosa nafasi katika diski hiyo. Lakini miaka kadhaa baadae katika eneo la on Sesame Street Bennett aliimba wimbo huo na ukiwa na mashairi ya kuiga yanayoitwa Slimey to the Moon katika mfululizo ambao msanii wa wimbo huu Slimey the Worm
Wimbo huu pia umekuwa ukiongoza katika mauzo ya kimataifa baada ya mwanamuziki Connie Francis kurekodi tar 28 Septemba 1962 katika lugha ya kilatini, na tar 23 Februari mwaka 1963 katika lugha ya kinepotalian huku matoleo yote yakitolewa na katika jina la Portami con te. Toleo katika lugha ya kuhispania lilirekodiwa tar 21 Februari 1963 na kuwa na jina la Llévame a la luna, japokuwa rekodi hii ilitolewa tena katika jina la Mandame a la luna.
Wanamuziki wa The Sandpipers pia walirekodi wimbo huu katika lugha ya Kihispania katika albamu yao ya mwaka 1967, iliyoitwa, Misty Roses. Wimbo huu pia ni maarufu nchini Ujerumani na umerekodiwa na wanamuziki kama vileTom Gabel katika albamu yake ya ‘’The Unknown’’ ya mwaka 2003, na pia na mwanamuziki mwingine Roger Cicero kama m"Schiess mich doch zum Mond" katika albamu yake ya Männersachen ya mwaka (2006). Wimbo huu ulifika katika hatua nyimgine baada ya kutumiwa katika ufunguzi wa filamu ya Oliver Stone's 1987 film Wall Street na pia umejumuishwa katika kuchangisha pesa kwa kundi la [[Allow Us to Be Frank.
Wimbo huu umesharudiwa na wasanii wengi hata katika nchi za Japan katika tamthilia ya Neon Genesis Evangelion
Mwaka 2000, Utada Hikaru alilimba pia wimbo huu wakati akitoa single yake ya Wait & See: Risk.Yi So-yeon, mwanaanga kutoka nchini Korea ya Kusini, alisema kuwa, alipokuwa angani aliimba wimbo huu kwa ajili ya wananga wenzake wakati walipokuwa angani.
Tarehe, 20 Julai 2009 wimbo huu pia uliimbwa na Diana Krall katika jubilee ya miaka 40ya Apollo 11 katika sherehe zilizofanyika katika makumbusho ya Smithsonian Air and Space Museum. Ambapo wanaanga watatu kutoka Apollo 11 mission ndio waliokuwa watazamaji..
Mwezi Oktoba 2009, kisehemu cha wimbo huu, kilitokezea katika mfano katika albamu ya DJ Lord Vampirick iliyoitwa "Straight Shotgun At The Edge Of The Universe". Wimbo huu pia umetokezea katika tamthilia ya nchini Korea ya kusini iliyoitwa You're Beautiful, uliimbwa na Tae Kyung (portrayed by Jang Geun Suk).