Feroza Adam

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Feroza Adam
Amezaliwa 16, agosti, 1961
Johannesburg, Afrika ya kusini
Amekufa 9, agosti, 1994

Feroza Adam, (16 Agosti, 19619 Agosti, 1994) alikuwa mwanaharakati wa kisiasa wa Afrika Kusini, mtangazaji wa African National Congress na mashirika mengine. Alichaguliwa kwenye Bunge mnamo mwaka 1994, muda mfupi kabla ya kufariki kwa ajali ya gari.

Maisha ya Awali[hariri | hariri chanzo]

Feroza Adam alilelewa katika kitongoji cha Lenasia, Johannesburg, katika familia ya Kiislamu. Alisoma katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand, ambako alijishughulisha na siasa kama mwanachama wa vikundi vya wanafunzi vilivyoshirikiana na shirika la Transvaal Indian Congress . Alifanya kazi katika bodi ya utendaji ya Shirika la Wanafunzi wa Azania. Baadaye sana aliedelea na masomo zaidi ya uhusiano wa kimataifa na diplomasia katika Taasisi ya Mahusiano ya Kimataifa ya Clingendael, nchini Uholanzi. [1]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Feroza Adam alifundisha shule baada ya kumaliza chuo. Alijiunga na shirikisho la wanawake wa Transvaal (Federation of Transvaal Women /FEDTVAW) na shirikisho la wanawake wa Afrika Kusini (Federation of South African Women), na tangu mwaka 1984 hadi 1990 alitumikia shirikisho la mwisho kama mtangazaji. Kuanzia 1988, alifanya kazi kwa wakati wote kwenye United Democratic Front . Alisaidia kuanzisha ofisi ya kikanda ya African National Congress kwa Pretoria-Witwatersrand-Vereeniging, na alifanya kazi katika kamati ya uongozi ya Muungano wa Kitaifa wa Wanawake . Alikuwa katibu wa utangazaji wa Ligi ya Wanawake ya ANC tangu 1992 hadi 1993. [2] Mnamo 1990, alitoa hotuba kwenye mkutano wa kitaifa wa wanawake, na akasema:

"Ni muhimu kwetu kuwaunganisha wanawake waliojitolea kwa Afrika Kusini ya kidemokrasia isiyo na ubaguzi wa rangi, wala ubaguzi wa kijinsia. Vinginevyo tutajikuta katika hali sawa na wanawake kutoka nchi nyingine katika zama za baada ya ukombozi. Baada ya kuhangaika pamoja na wanaume wao kwa ajili ya ukombozi, wanawake wandugu walipata msimamo wao haujabadilika. Tunahitaji kusisitiza msimamo wetu kama wanawake kwa nguvu zaidi sasa kuliko hapo awali, na tunaweza tu kufanya hivyo kama sauti moja, yenye umoja na ukubwa." [3]

Mnamo 1994, alichaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Kitaifa, katika serikali ya kwanza iliyochaguliwa kidemokrasia nchini Afrika Kusini . [4]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Feroza Adam" South African History Online (17 February 2011).
  2. "Celebrating the Life of Feroza Adam" UNISA (6 August 2013).
  3. Quoted in Shamim Meer, "Freedom for Women: Mainstreaming Gender in the South African Liberation Struggle and Beyond" Gender and Development 13(2)(July 2005): 36.
  4. Fiona Wallace, "In Memory of Feroza Adam" Agenda: Empowering Women for Gender Equity 23(1994): 108.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Feroza Adam kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.