Fábio Carvalho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Carvalho akiichezea Liverpool mwaka 2022

Fábio Leandro Freitas Gouveia Carvalho (alizaliwa 30 Agosti 2002 ni mchezaji wa mpira wa miguu wa kulipwa wa Ureno, ambaye anacheza kama winga au kiungo mshambuliaji katika klabu ya Liverpool F.C..

Carvalho ni Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa vijana wa Uingereza, Carvalho sasa anaiwakilisha Ureno kimataifa katika michezo ya wenye umri wa chini ya miaka 21.

Maisha yake na ndoto[hariri | hariri chanzo]

Carvalho alizaliwa huko Torres Vedras, katika Wilaya ya Lisbon nchini Ureno.[1]Alizaliwa na baba wa Angola na mama wa Kireno.[2] Alicheza katika akademi ya vijana ya 'Olivais Sul na Benfica kabla ya kuhamia na familia yake London nchini Uingereza mnamo 2013. [3][1] Aliichezea Balham kabla ya kusajiliwa na Fulham mnamo 2015.[4]

Maisha ya kazi[hariri | hariri chanzo]

Fulham[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Mei 2020, Carvalho alisaini mkataba wake wa kwanza wa kikazi na Fulham, wa miaka miwili.[5] Mnamo tarehe 23 Septemba, Carvalho alicheza mechi yake ya kwanza katika kikosi cha kwanza kama mchezaji wa akiba katika ushindi wa 2-0 wa Kombe la EFL dhidi ya Sheffield Wednesday.[6] Mnamo tarehe 15 Mei 2021, Carvalho alifunga bao lake la kwanza katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Southampton.[7]

Carvalho alianza vyema msimu wa 2021-22, akifunga mabao matatu katika mechi zake tano za kwanza huku Fulham wakitarajia kurejea tena katika Ligi Kuu. Kwa matokeo hayo, Carvalho alitunukiwa mchezaji bora wa mwezi wa EFL kwa Agosti 2021.[8]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Fernandes, Mariana. "Fábio Carvalho, o miúdo português capitão de Inglaterra que está a dar nas vistas no Fulham", 11 October 2018. (pt) 
  2. "From street football to childhood emigration: the background on Liverpool’s Portuguese newcomer Fábio Carvalho". portugoal.net. 
  3. "Moldado na Zona J, passou pelo Benfica e faz Klopp suspirar". Maisfutebol. 
  4. Wright, Nick. "Fabio Carvalho to Liverpool: Fulham's rising star long destined for the top", 3 February 2022. 
  5. "Fabio Carvalho goes pro". Fulham F.C. 22 May 2020. Iliwekwa mnamo 24 September 2020.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  6. "Fulham 2–0 Sheffield Wednesday", 23 September 2020. 
  7. Beardmore, Michael. "Southampton 3–1 Fulham: Che Adams, Nathan Tella & Theo Walcott earn Saints back-to-back wins", 15 May 2021. 
  8. "Fabio Carvalho named EFL's Young Player of the Month for August". English Football League. 14 September 2021. Iliwekwa mnamo 21 October 2021.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fábio Carvalho kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.