Eukeri wa Orleans

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kifo chake kinavyoonyeshwa katika dirisha la kioo cha rangi.

Eukeri wa Orleans (Orleans, leo nchini Ufaransa, 687 hivi - Sint-Truiden, leo nchini Ubelgiji, 743) alikuwa askofu wa mji huo wa Gaul (leo Ufaransa) kuanzia mwaka 721 hadi 733 hivi.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Februari[1].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Kisha kusoma nyaraka za Mtume Paulo, alitawa katika monasteri ya Jumieges.

Baada ya miaka saba, kutokana na sifa zake, alichaguliwa kuwa askofu wa Orleans lakini alisingiziwa kwa Karolo Nyundo ambaye, kisha kupata ushindi katika Mapigano ya Tours na Poitiers, alimpeleka uhamishoni Cologne, leo nchini Ujerumani. Hata hivyo, alipoona amepokewa vizuri mno, aliomba kwenda kuishi katika monasteri alimofariki baadaye[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Lives of the Saints: For Every Day of the Year; edited by Rev. Hugo Hoever, S.O.Cist., Ph.D., New York: Catholic Book Publishing Co., 1955

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.