Eujeni wa Karthago

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Eujeni wa Karthago (alifariki 483) alikuwa askofu wa mji huo (leo nchini Tunisia) hadi alipopelekwa uhamishoni katika kisiwa cha Corsica (leo nchini Ufaransa) kutokana na dhuluma za Wavandali Waario dhidi ya Wakatoliki. Ilikuwa vilevile kwa maaskofu wengine 650.

Baada ya kuinjilisha kisiwa hicho pamoja na maaskofu Vendemiale na Lonjino wa Pamaria, hatimaye alifia dini.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Mei[1].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.