Nenda kwa yaliyomo

Eneo la vijijini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eneo la mashambani Australia lenye kilimo cha mizabibu.
Kijiji cha Amra Kalan, Pakistan, kinachofanana na mji mdogo.
Pori asilia mara nyingi huhesabiwa kati ya maeneo ya vijijini, hata kama hakuna kijiji.

Eneo la vijijini (kwa Kiingereza: rural area, countryside) ni eneo ambalo si mji wala jiji. Mara nyingi ni eneo la kilimo au mashamba. Kwa hiyo watu husema pia "mashambani". Wakazi wake wanaoishi humo hukaa katika vitongoji au vijiji; wakati mwingine pia sehemu pasipo nyumba nyingine.

Kwa kawaida maeneo ya vijijini hakuna msongamano mkubwa wa watu na makazi hayana nyumba nyingi kama mji.

Vijijini ni kinyume cha neno "mjini" linalomaanisha eneo ambako majengo ni mengi na watu wengi hukaa pamoja.

Nchi nyingi zinafafanua "maeneo ya vijijini" kwa matumizi ya kitakwimu lakini fafanuzi hizi zinatofautiana.

  1. Huko Uhindi eneo la vijijini linafafanuliwa kuwa na msongamano wa watu chini ya 400 kwa kilomita ya mraba, na wanaume asilimia 75 wanafanya kazi ya kilimo[1].
  2. Kanada eneo la vijijini linafafanuliwa kuwa na msongamano wa watu chini ya 150 kwa kilomita ya mraba.
  3. Pakistan kila eneo nje ya mipaka ya manisipaa linatazamwa kuwa la vijijini.[2]

Kisheria kuna tofauti kati ya maeneo ya mjini (urban) na vijijini (rural) kwenye nchi tofauti kuhusu kiwango cha madaraka ya kujitawala, kiasi cha fedha kinachopangiwa kwa matumizi ya serikali, ubora wa miundombinu, huduma na kadhalika. Mara nyingi vijijini umaskini ni mkubwa kuliko mjini.

  1. "In Focus" (PDF). www.dhanbank.com. Desemba 2010. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2020-02-02. Iliwekwa mnamo 2019-12-04.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Zaidi, S. Akbar (29 Agosti 2017). "Rethinking urban and rural". Dawn.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Simple English Wiktionary
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina dictionary definitions (word meanings):
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Eneo la vijijini kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.