Eliaquim Mangala

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mangala akiwa Manchester City.

Eliaquim Hans Mangala (alizaliwa 13 Februari 1991) ni mchezaji wa soka wa Ufaransa ambaye anachezea klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Ufaransa kama mlinzi wa kati.

Alizaliwa nchini Ufaransa, alihamia Ubelgiji akiwa mtoto na kuanza kazi yake huko Standard Liège, akaenda FC Porto mwaka 2011 ambapo alishinda mfululizo Premierira Liga kabla ya kujiunga na Manchester City mwaka 2014 kwa £ milioni 32.

Mangala aliisaidia timu yake na timu yake ya taifa ya Ufaransa tarehe 6 Juni 2013 dhidi ya Uruguay. Alijumuishwa katika kikosi cha timu hiyo katika Kombe la Dunia la 2014 na Euro 2016, aliisaidia timu yake kushika nafasi nzuri katika mashindano hayo.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Eliaquim Mangala kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.