Edwin Hubble

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Edwin Hubble
Edwin Hubble

Edwin Powell Hubble (20 Novemba 1889 - 28 Septemba 1953) alikuwa mwanaastronomia wa Marekani. Matokeo ya Hubble yalibadilisha mwono wa kisayansi wa ulimwengu.

Mnamo 1926 alionyesha kwamba mawingu angavu kwenye anga zilizoitwa tu "nebula" hadi wakati ule hali halisi ni galaksi kama hii ya dunia yetu, Njia Nyeupe. Pia, alitunga mfumo wa kuainisha galaksi[1].

Kisha akaonyesha kuwa galaksi zilikuwa zikipishana. Hubble iligundua kiwango cha athari ya Doppler (redshift) kutoka kwenye galaksi iliongezeka kulingana na umbali wake kutoka duniani.

Mwaka wa 1929 Hubble aliunda kile kinachoitwa kanuni ya Hubble. Kanuni inasema kuongezeka kwa umbali kati ya galaksi mbili yoyote kunalingana na kasi kubwa zaidi ya kutengana. Maana yake galaksi zote zina mwendo wa kuongeza umbali kati yao na hii iliweka msingi wa nadharia ya kwamba ulimwengu wote unapanuka. Hubble hakuwa wa kwanza wa kuwaza nadharia hii alitanguliwa na Georges Lemaître aliyewahi kuibuni na kutangaza miaka miwili kabla lakini jarida aliyotumia haikujulikana sana.

Darubini ya Hubble ilipokea jina kwa heshima yake.

Marejeo

  1. Hubble, Edwin (December 1926). "Extragalactic nebulae" , Astrophysical Journal. 64 (64): 321–369, tovuti ya Chuo Kikuu cha Harvard, SAO/NASA ADS Astronomy Abstract Service, iliangaliwa Aprili 2018
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Edwin Hubble kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.