Nenda kwa yaliyomo

Edward Snowden

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Edward Snowden

Nchi Marekani
Kazi yake Bingwa wa kompyuta

Edward Joseph Snowden (/ ˈsnoʊdən/; amezaliwa Elizabeth City, North Carolina.[1], 21 Juni 1983[2]) ni mshauri wa zamani wa ujasusi wa kompyuta wa Marekani ambaye alivujisha taarifa za siri zilizoainishwa kutoka kwa Wakala wa Usalama wa Kitaifa (NSA) ya huko Marekani mnamo mwaka 2013, alipokuwa mfanyakazi na mkandarasi mdogo. Ufichuzi wake huo ulionyesha na kuelezea programu nyingi za uchunguzi wa kimataifa, nyingi zinazoendeshwa na NSA na Muungano wa mashirika matano ya ujasusi kwa ushirikiano wa makampuni ya mawasiliano ya simu na serikali za Ulaya, na kuibua mjadala mkubwa kuhusiana na usalama wa taarifa na faragha ya mtu binafsi.

Mnamo mwaka 2013,Snowden aliajiriwa katika shirika la NSA na Booz Allen Hamilton baada ya kufanya kazi na Dell na CIA[3].Snowden anaeleza kuwa hakupendeza na programu zilizo kuwa zikiendeshwa, na hivyo kutafuta utatuzi wa kimaadili na kisheria na kukosa ufumbuzi.Mnamo machi 20 2013 snowden alisafiri hadi Hong Kong baada ya kuacha kazi yake huko NSA Hawaii na mwanzoni mwa juni kuvujisha nyaraka za siri sana za serikali ya marekani kwa wanahabari Glenn Greenwald, Laura Poitras, Barton Gellman, na Ewen MacAskill. Snowden alikuja kufahamika sana kimataifa baada ya chapisho la gazeti la The Guardian, The Washington Post, na machapisho mengine. Snowden alitoa malalamiko mengi kuhusiana na shirika la serikali la usalama wa mawasiliano (GCSB) la huko Nyuzilandi. Aliwatuhumu kwa kufanya shughuli za ufuatiliaji wa wananchi wa New Zealand na kujihusisha na ujasusi kati ya mwaka 2008 na 2016, kipindi ambacho waziri mkuu John Key alishika hatamu.[4][5]

Mnamo Juni 21 mwaka 2013, Idara ya Haki ya Marekani ilifungua mashtaka dhidi ya Snowden, kutokana na makosa mawili ya ukiukwaji wa sheria ya Ujasusi ya mwaka 1917[6] na uwizi wa nyaraka za serikali, pia kuongozana na kufungia pasipoti yake[7].Siku mbili baadae alisafiri kwa ndege hadi kiwanja cha kimataifa cha ndege cha Moscow Sheremetyevo,na ambapo uongozi wa urusi uliangalia pasipoti yake na kumnyima kutoka kiwanjani kwa muda wa zaidi ya mwezi mzima akiwa kiwanjani hapo. Urusi baadae ilimpatia snowden kibali cha kidiplomasia cha kukaa nchini humo kama raia wa kawaida asiye na kosa lolote, kibali chenye muda wa mwaka mmoja na kuweza kuongezwa pindi atakapo. Mnamo oktoba 2020 alipatiwa kibali rasmi cha kukaa milele kama raia ya kawaida huko chini urusi. Septemba 2022 snowden alikabidhiwa nyaraka za kuwa raia wa nchini humo na raisi Vladimir Putin na mnamo disemba 2 mwaka huo huo aliapa kiapo cha utiifu na chini hio.[8]

Suala la utata ni kwamba Snowden amekuwa akisifiwa na kulaaniwa kwa kitendo chake hichi cha kuvujisha siri za mashirika ya usalama ya marekani,na hivyo snowden amekuwa akijitetea katika hali ya kuelezea umma kuwa amefanya hivyo ili jamii na watu duniani ni vitu gani vimekuwa vikifanyika bila ridhaa zao. Ufichuzi wake umechochea mijadala juu ya ufuatiliaji wa watu, usiri wa serikali, na uwiano kati ya usalama wa taifa na faragha ya habari, jambo ambalo amesema alikusudia kufanya katika mahojiano ya awali na vyombo tofauti tofauti vya habari.

Mwanzoni mwa mwaka 2016 Snowden alikuwa raisi wa shirika lililojulikana kama Freedom of the Press,lilikuwa ni shirika lisilo kuwa la kibiashara kutokea mjini San Fransisco, ambalo lilikuwa likijihusisha na kuwalinda wanahabari na wahariri kutokana na kudukuliwa na vitengo vya uchunguzi vya serikali.[9] Mwaka 2017, snowden alifunga ndoa na mwanadada Lindsay Mills."Nililaza kichwa changu huko Moscow kwenye mto wakati wa usiku," aliiambia hadhira ya Israeli mnamo Novemba 2018, "Huku nikiishi kwenye mitandao na katika kila jiji lingine ulimwenguni."[10] Mnamo septemba 17,2019 kumbukumbu ya Edward Snowden ilichapishwa.[11] Kufikia 2 Septemba 2020 Mahakama ya shirikisho ya Marekani iliamua kuwa mpango wa taasisi ya Ujasusi marekani ya ufuatiliaji wa watu ikiwemo wananchi wa kawaida uliofichuliwa na Snowden haukuwa wa halali na pengine ulikuwa kinyume na katiba ya Marekani [12]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. "Report: Snowden has document to enter Russia", WVEC, July 24, 2013. Retrieved on 2023-03-07. Archived from the original on 2013-08-22. "Edward Snowden, who was born in Elizabeth City, NC, is wanted in the U.S. for espionage" by the FBI et al." 
 2. Ackerman, Spencer. "Edward Snowden was not successful in joining the US Army's elite special forces unit", The Guardian, June 10, 2013. "The army did confirm Snowden's date of birth: 21 June 1983." 
 3. Condé Nast (2014-04-23). "Snowden Speaks: A Vanity Fair Special Report". Vanity Fair (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-02-24.
 4. Glenn GreenwaldRyan GallagherGlenn Greenwald, Ryan GallagherSeptember 15 2014, 4:33 A.m. "New Zealand Launched Mass Surveillance Project While Publicly Denying It". The Intercept (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-03-03.{{cite web}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link)
 5. Keck, Zachary. "Edward Snowden Vs New Zealand". thediplomat.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo Machi 4, 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 6. Finn, Peter; Horwitz, Sari (2013-06-21), "U.S. charges Snowden with espionage", Washington Post (kwa American English), ISSN 0190-8286, iliwekwa mnamo 2023-03-03
 7. "Kerry warns Russia on Snowden: "Respect the relationship"". www.cbsnews.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-03-03.
 8. https://www.washingtonpost.com/world/2022/12/02/edward-snowden-russian-citizenship/
 9. Kigezo:Cite magazine
 10. "Snowden's book doesn't mention a job at 'one of Russia's biggest websites,' and former CIA officials suspect a darker reality". finance.yahoo.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo Julai 9, 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 11. McAskill, Ewan. "I was very much a person the most powerful government in the world wanted to go away", The Guardian, September 13, 2019. 
 12. "U.S. court: Mass surveillance program exposed by Snowden was illegal", Reuters, September 2, 2020. 
 13. Jessica, Corbett. "Edward Snowden Anashiriki Hadithi Yake katika Kumbukumbu Mpya Inayoonyesha Rafu Mwezi Septemba". Ndoto za Kawaida. {{cite web}}: Unknown parameter |access -date= ignored (help); Unknown parameter |tarehe= ignored (help)
 14. [https:// ew.com/books/2019/08/01/edward-snowden-memoir-permanent-record/ "Edward Snowden atangaza kumbukumbu ya 'Rekodi ya Kudumu' kwa ajili ya toleo la kuanguka"]. EW.com. Iliwekwa mnamo Agosti 2, 2019. {{cite web}}: Check |url= value (help)

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]