Nenda kwa yaliyomo

Mwanahabari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wanahabari)
Mwandishi wa runinga akiwa ameshika mikrofoni.
Wanahabari wapiga picha wakati wa mechi ya kandanda.

Mwanahabari ni mtu anayefanya kazi ya uandishi wa habari akikusanya, kutayarisha na kusambaza habari. Anaweza kufanya kazi hiyo akiwa ameajiriwa na gazeti, redio au kituo cha televisheni au kama mkandarasi wa kujitegemea akiuza kazi yake kama makala, picha au filamu. Wanahabari huajiriwa pia na makampuni, taasisi au ofisi za serikali zinazolenga kueleza kazi yao katika jamii.

Akiwa mwandishi wa habari wa gazeti huandika nakala za habari na hadithi kwa magazeti. Katika maandalizi ya makala ataongea na watu, kufuatilia habari kwa jumla, kufanya utafiti na mahojiano na watu wanaohusika katika habari anayoandaa. Akiona kuna tofauti jinsi gani tukio au tatizo linatazamwa na watu atajaribu kuonyesha pande zote mbili.

Sehemu ya kazi yake ni pia kutoa maoni kuhusu yale anayoripoti. Kwa kawaida anatakiwa kutenganisha taarifa za habari na maoni yake kuhusu watendaji au namna ya utendaji, lakini hali halisi si rahisi kutenganisha pande hizo mbili.

Hatari za kazi

[hariri | hariri chanzo]
Hali ya uhuru wa uandishi habari duniani 2021 (Press Freedom Index 2021)
Hali nzuri - Hali ya kuridhika - Matatizo dhahiri - Hali ngumu - Hali ngumu sana

Wakati mwingine kazi yao inaingiza wanahabari hatarini. Hii inatokea hasa wakifanya ripoti katika maeneo ya vita au mapigano makali, lakini pia wakifanya kazi katika maeneo ambako uhuru wa uandishi habari hauheshimiwi au vikundi vya wahalifu wakati wanataka kuzuia habari juu ya matendo yao.

Ingawa nchi karibu zote zimekubali Azimio la Kimataifa juu ya Haki za Binadamu ambamo Kifungu cha 19 inasema "Kila mmoja ana haki ya uhuru wa kutoa na kueleza maoni yake; haki hii inahusu pia uhuru wa kushikilia maoni yake bila kuingiliwa kati na uhuru wa kutafuta na kutoa habari na maoni kwa njia yoyote bila kujali mipaka", hali halisi nchi nyingi hazifuati kanuni hizo. Kufuatana na Kamati ya Kimataifa ya Kulinda Wanahabari (Committee to Protect Journalists) kwenye mwaka 2010 wanahabari 251 walikuwa wamefungwa jela kwa kazi yao [1] Nchi zenye wanahabari wengi katika jela ni: Uturuki (95), Jamhuri ya Watu wa China (34), Iran (34), Eritrea (17), Myanmar (13), Uzbekistan (6), Vietnam (5), Kuba (4), Ethiopia (4) na Sudan (3).[2]

Wanahabari wanauawa pia kazini. Katika mwaka 2019 wanahabari 16 waliuawa kazini katika miezi 9 hadi Oktoba: 5 nchini Meksiko na 2 Somalia. 9 waliuawa ili kulipiza kisasi kuhusu taarifa zao au kuwazuia wasiendelee, wengine waliripoti kutoka mapambano ambako silaha zilitumiwa wakipigwa risasi.[3]

  1. Hundreds of journalists jailed globally becomes the new normal, tovuti ya Committee to Protect Journalists, iliangaliwa Oktoba 2019.
  2. Iran, China drive prison tally to 14-year high. "Iran, China drive prison tally to 14-year high (December 8, 2010). Committee to Protect Journalists. Retrieved November 18, 2011". Cpj.org. Iliwekwa mnamo 2013-04-16.{{cite web}}: CS1 maint: numeric names: authors list (link)
  3. 16 journalists killed in 2019, motives confirmed tovuti ya Committee to Protect Journalists, iliangaliwa Oktoba 2019.

Marejeo mengine

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwanahabari kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.