Edward Cummings

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Edward Cummings

Edward Estlin Cummings (14 Oktoba 1894 - 3 Septemba 1962), au kwa kifupi e.e. cummings, alikuwa mshairi na mwandishi mashuhuri kutoka Marekani. Kwa jumla aliandika na kuchapisha mashairi, riwaya na tamthilia mia tisa. Vile vile, Cummings alijulikana sana kama mchoraji maarufu aliyechora picha kadhaa zilizovutia.

Mashairi ya Cummings yaligusia sana maswala ya mapenzi na mazingira - alipenda sana kuandika juu ya msimu wa "spring". Mashairi yake yalipata umaarufu kwa sababu hayakuakifishwa kama ilivyo kawaida.

Watalaamu wengi wanaamini kuwa Cummings alikuwa mmojawapo wa washairi waliojulikana sana kule Marekani katika karne iliyopita. Mashairi aliyoandika Cummings, na ambayo yanajulikana sana, ni kama "in just spring", "a man who had fallen amongst thieves", "the cambridge ladies" na "Buffalo Bill".