Nenda kwa yaliyomo

Mapito ya Drake

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Drake Passage)
Ramani ya Drake Passage.
Mpito na visiwa vya Falkland Islands, South Georgia Islands na South Sandwich Islands.

Mapito ya Drake (kwa Kiingereza: Drake Passage; kwa Kihispania: Estrecho de Magallanes) ni sehemu ya maji inayounganisha Bahari Atlantiki (hasa sehemu ya Bahari ya Scotia) na Bahari Pasifiki. Upande wa kaskazini iko Rasi ya Hoorn na Amerika Kusini, upande wa kusini viko Visiwa vya South Shetland ambavyo viko mbele ya pwani ya Antaktiki. Sehemu za kusini za maji huhesabiwa kuwa ndani ya Bahari ya Antaktiki.

Jina linatokana na nahodha Mwingereza Francis Drake aliyezunguka Amerika Kusini katika mwaka 1578. Drake mwenyewe alitumia mlangobahari wa Magellan lakini baada ya kufika katika Pasifiki alisukumwa na dhoruba mbali upande wa kusini akahisi kuna mpito hapa unaoruhusu kufika Atlantiki. Jahazi la kwanza linalojulikana kutumia Mpito wa Drake lilikuwa "Edndracht" wa Uholanzi katika mwaka 1616, na kwenye nafasi hii Rasi ya Hoorn ilipokea jina lake.

Sehemu hii ya bahari ni maarufu kwa sababu ya ukali wa mawimbi yake yanayofikia hadi kimo cha mita 10.

Katika vitabu vya kale vya Kiingereza jina linatajwa pia kuwa "Drake Strait" yaani mlangobahari wa Drake, lakini upana wake wa kilomita 800 ni mkubwa mno kwa ufafanuzi wa "mlangobahari".

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]