Mapito ya Drake
Mapito ya Drake (kwa Kiingereza: Drake Passage; kwa Kihispania: Mar de Hoces = Bahari ya Hoces) ni sehemu ya maji inayounganisha Bahari Atlantiki (hasa sehemu ya Bahari ya Scotia) na Bahari Pasifiki. Upande wa kaskazini iko Rasi ya Hoorn na Amerika Kusini, upande wa kusini viko Visiwa vya South Shetland ambavyo viko mbele ya pwani ya Antaktiki. Sehemu za kusini za maji huhesabiwa kuwa ndani ya Bahari ya Antaktiki.
Jina linatokana na nahodha Mwingereza Francis Drake aliyezunguka Amerika Kusini katika mwaka 1578. Drake mwenyewe alitumia mlangobahari wa Magellan lakini baada ya kufika katika Pasifiki alisukumwa na dhoruba mbali upande wa kusini akahisi kuna mpito hapa unaoruhusu kufika Atlantiki. Jahazi la kwanza linalojulikana kutumia Mpito wa Drake lilikuwa "Edndracht" wa Uholanzi katika mwaka 1616, na kwenye nafasi hii Rasi ya Hoorn ilipokea jina lake.
Sehemu hii ya bahari ni maarufu kwa sababu ya ukali wa mawimbi yake yanayofikia hadi kimo cha mita 10.
Katika vitabu vya kale vya Kiingereza jina linatajwa pia kuwa "Drake Strait" yaani mlangobahari wa Drake, lakini upana wake wa kilomita 800 ni mkubwa mno kwa ufafanuzi wa "mlangobahari".
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- National Oceanography Centre, Southampton page of the important and complex bathymetry of the Passage Ilihifadhiwa 2 Julai 2010 kwenye Wayback Machine.
- A personal story describing crossing the Passage Ilihifadhiwa 7 Oktoba 2013 kwenye Wayback Machine.
- A NASA image of an eddy in the Passage Ilihifadhiwa 4 Desemba 2004 kwenye Wayback Machine.
- Larger-scale images of the passage from the US Navy (Rain, ice edge and wind images) Ilihifadhiwa 23 Oktoba 2004 kwenye Wayback Machine.
- BBC News story on a scientific study dating the age of the Drake Passage