Dotto Rangimoto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Dotto Rangimoto (amezaliwa 2 Agosti 1986) ni mwandishi wa mashairi na riwaya kutoka nchini Tanzania. Dotto ni mshindi mara mbili wa tuzo ya fasihi ya Mabati Cornell. Alishinda katika kipengele che ushairi 2017 huku kipengele cha riwaya kwa mwaka wa 2022.

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Dotto Rangimoto amezaliwa tarehe 2 Agosti 1986 pamoja na pacha wake Kurwa Rangimoto, katika mkoa wa Morogoro kwa wazazi Daudi Rangimoto na Rehema Chamchua.

Taaluma[hariri | hariri chanzo]

Dotto Rangimoto alimaliza Shule ya Msingi Chamwino; Morogoro mwaka 1999. Aliendelea na masomo ya sekondari katika shule ya Morogoro Sekondari na kufanikiwa kumaliza elimu yake ya sekondari mwaka 2004 akiwa na ufaulu mzuri huku akipata alama "A" katika somo la hisabati, yaani "Basic Mathematics" ambalo alikuwa akilimudu vizuri tangu akiwa elimu ya msingi.

Kujihusisha na utunzi wa mashairi na riwaya[hariri | hariri chanzo]

Ni mtunzi wa mashairi ya kimapokeo aliyefanikiwa kunyakua tuzo kadhaa za kitaifa na za kimataifa katika uandishi wa mashairi na fasihi ya Kiswahili.

Mwaka 2018 alitangazwa mshindi wa tuzo ya kimataifa ya fasihi ya Kiswahili ya Mabati Cornell Award baada ya kushinda katika uandishi wa shairi lake liitwalo "Mwanangu Rudi Nyumbani".[1]

Pia, Rangimoto ametoa diwani iitwayo jina hilo hilo. Mwaka wa 2022, alitoa riwaya yake ya kwanza yenye jina la Wivu wa Bustani ya Edeni. Mwaka wa 2023, akatoa riwaya yake ya pili yenye jina la Nakupenda Jini Maimuna. Hizo ndizo riwaya zake pekee hadi sasa. Pia Dotto ni mwandishi pekee aliyeshinda mara mbili katika tuzo za Mabati kwa tanzu mbili tofauti. Ushairi 2017, riwaya 2022.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "2017 Winners". kiswahiliprize.cornell.edu (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2018-08-20. 
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dotto Rangimoto kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.