Doris Mollel

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Doris Mollel (alizaliwa jijini Dar es Salaam, 3 Desemba 1990) ni mwanzilishi na mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Foundation inayojihusisha na kusaidia watoto wanaozailiwa kabla ya wakati yaani njiti.

Maisha yake[hariri | hariri chanzo]

Doris Mollel alizaliwa njiti pamoja na pacha wake David, wakiwa ni wa kwanza kuzaliwa katika familia ya watoto watatu ya William Mollel (Marehemu) na Mama Celine Mollel. Amekuwa akijibidiisha kutoa misaada mbalimbali kwa jamii kupitia taasisi yake ya Doris Foundation, misaada hiyo ni pamoja na vifaa tiba katika hospitali mbalimbali nchini Tanzania kwa kushirikiana na wadau [1] lakini pia kusaidia upatikanaji wa mahitaji muhimu kwa ajili ya watoto Njiti kama vile, Mashine za Oksijeni na za kunyonyea uchafu kutoka kwa watoto Njiti[2] lakini pia kuwasaidia wazazi wa watoto hao pale msaada unapohitajika[3]

Elimu yake[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2008 alihitimu kidato cha nne katika sekondari ya Umoja na baadaye kidato cha sita katika shule ya sekondari ya wasichana ya tabora na Mwaka, 2012 alijiunga na chuo kikuu cha Mwalimu Nyerere ambapo alikuwa akisomea shahada ya Siasa na Usimamizi wa Maendeleo ya Jamii.[4]

Kazi yake[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 2015 Doris Foundation ilizinduliwa rasmi na Doris akiwa mkurugenzi wa taasisi.

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 2012 Doris alifanikiwa kutwaa taji mrembo wa utalii katika chuo cha Mwalimu Nyerere na kitu cha kwanza kufanya baada ya kuchaguliwa huko ni kupeleka watoto yatima wa kituo cha Chakuwama, Sinza, Dar es Salaam kwenda kuona vituo vya utalii mjini Bagamoyo. Mwaka 2013 aliweza kushinda katika mashindano ya Urembo ya REDDS MISS ILALA 2013[5] Mnamo mwaka 2014 alishiriki mashindano ya mrembo wa Singida na kutwaa taji la Miss Singida 2014[6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]