Nenda kwa yaliyomo

Divock Origi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Origi akiwa Liverpool.

Divock Okoth Origi (alizaliwa 18 Aprili 1995) ni mchezaji wa soka wa Ubelgiji ambaye anacheza kama mshambuliaji wa klabu ya Liverpool FC na timu ya taifa ya Ubelgiji.

Origi ana asili ya Kenya: ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa kitaifa wa Kenya Mike Origi ambaye ni wa jamii ya Waluhya.

Origi alianza kazi yake ya kucheza mpira wa miguu katika akademia ya vijana wa Genk ambako alitumia miaka tisa na baadae kusaini Lille 2010, akiwa na umri wa miaka 19 alikataa maombi ya kusaini mkataba na Manchester United F.C. kwa sababu zisizojulikana.

Tarehe 29 Julai 2014, klabu ya Liverpool ilisaini mkataba wa miaka mitano kwa £ milioni 10. Mkataba wake utaisha mwishoni mwa msimu wa 2019-20.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Divock Origi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.