Ugonjwa
Mandhari
(Elekezwa kutoka Disease)
Ugonjwa au maradhi ni hali ya mvurugo katika utendaji wa kawaida wa shughuli za mwili na roho inayoathiri vibaya ustawi au starehe ya kiumbehai. Hivyo hakuna tofauti kamili baina ya ugonjwa na hali ya kujisikia vibaya.
Sayansi inayochungulia magonjwa ni sayansi ya tiba.
Magonjwa yanaweza kugawanyika kutokana na vyanzo/asili zake kama vile:
- magonjwa ya kuambukiza
- magonjwa ya kurithi
- magonjwa kutokana na ajali
- magonjwa kutokana na dutu za nje ya mwili (sumu, asidi) au moto
- magonjwa ya kansa
- magonjwa yaliyosababishwa na tiba
- magonjwa yaliyosababishwa na mfumo wa kingamaradhi uliomo mwilini
- magonjwa ya nafsi
- magonjwa ya roho
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ugonjwa kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |