Nenda kwa yaliyomo

Desiree wa Bourges

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Desiree wa Bourges (kwa Kilatini: Desideratus; Soissons, 512 - Bourges, 8 Mei 550) alikuwa askofu wa mji huo, leo nchini Ufaransa, aliyelipatia jimbo masalia ya wafiadini katika mwaka mmoja wa uongozi wake[1][2].

Kwanza alikuwa chansela wa mfalme Klotari I na kupambana na uzushi na usimoni. Alipotaka kuingia umonaki, mfalme alimuambia afadhali ahudumie watu wake[3].

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama mtakatifu, sawa na wazazi na ndugu zake wawili.

Sikukuu yake ni tarehe 8 Mei[4].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.