Daraja la Dona Ana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Daraja la Dona Ana
Kiingereza: Dona Ana Bridge
Kireno: Ponte Dona Ana
Yabeba Reli ya Sena
Yavuka Mto Zambezi
Mahali Vila de Sena, Msumbiji
Mbunifu wa mradi Edgar Cardoso
Urefu mita 3,670
Idadi ya nguzo 40
Yatanguliwa na Daraja la Samora Machel
Yafuatiwa na Daraja la Armando Emilio Guebuza
Anwani ya kijiografia 17°26′31″S 35°03′07″E / 17.44194°S 35.05194°E / -17.44194; 35.05194
Daraja la Dona Ana is located in Msumbiji
Daraja la Dona Ana

Daraja la Dona Ana ni daraja linalovuka Mto Zambezi nchini Msumbiji kati za miji za Mutarara na Sena. Likiwa na urefu wa kilomita 3.7 ni daraja defu la kuvuka Zambezi. Lilijengwa mnamo 1934 zamani za ukoloni wa Kireno kwa mvuko wa reli kwa kusudi la usafiri kati ya Malawi, migodi ya makaa mawe ya Mutarara na bandari ya Beira.

Wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Msumbiji daraja likaharibiwa na tangu 1995 kutengenezwa kwa usafiri wa magari. Tangu mwaka 2009 hutumiwa tena kwa usafiri wa reli.