Nenda kwa yaliyomo

Mtango

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Cucumis sativus)
Mtango
(Cucumis sativus)
Mtango shambani
Mtango shambani
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Cucurbitales (Mimea kama mboga)
Familia: Cucurbitaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mboga)
Jenasi: Cucumis
L.
Spishi: C. sativus
L.

Mtango (Cucumis sativus) ni mmea mtambaa wa familia Cucurbitaceae. Matunda yake, yaitwayo matango, hutumika sana katika saladi duniani kote.

Spishi mbili za pori huitwa mtango-mwitu (Cucumis aculeatus na C. dipsaceus). Lakini mtango-tamu (Solanum muricatum) hauna mnasaba na mtango, kwa sababu ni mwana wa familia Solanaceae.