Cuba Gooding, Jr.
Cuba Gooding, Jr. | |
---|---|
Gooding, Jr. mnamo Aprili 2022 | |
Amezaliwa | Cuba M. Gooding, Jr. 2 Januari 1968 |
Kazi yake | Mwigizaji/Mtayarishaji filamu |
Miaka ya kazi | 1987–mpaka sasa |
Ndoa | Sara Kapfer (13 Machi 1994) watoto wa 3 |
Cuba M. Gooding, Jr. (amezaliwa tar. 12 Januari 1968) ni mwigizaji filamu kutoka nchini Marekani. Anafahamika sana kwa ushindi wake Tuzo ya Academy-akiwa kama mwigizaji mwandamizi bora kwenye filamu ya Jerry Maguire ambamo kacheza kama Rod Tidwell mnamo 1996, akiwa sambamba kabisa na Tom Cruise. Pia anafahamika sana kwa kucheza kwenye filamu iliongozwa na John Singleton ya Boyz n the Hood mnamo mwaka wa 1991.
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Cuba Gooding, Jr. alizaliwa na kukulia mjini The Bronx, New York, akiwa kama mtoto wa Shirley, mwimbaji mwenye sauti Nyororo, na Cuba Gooding, Sr., mwimbaji kiongozi wa kundi la muziki wa soul la The Main Ingredient.[1] Ana ndugu wa kiume wawili, mwanamuziki Tommy Gooding na mwigizaji mwenzi wake Omar Gooding. Familia yake ilihamia mjini Los Angeles baada ya kundi la Mzee wake kupata kibao chao kikali "Everybody Plays the Fool" mnamo mwaka wa 1972; halafu mzee wake akajitia kuitelekeza familia yake baada ya miaka miwili baadaye. Wakati wa kuonekana kwake kwenye Baada ya kuonekana kwake kwenye The Howard Stern Show, Gooding akagundua kwamba baada ya baba yake kuondoka, familia yake ilikuwa ikiishi kwenye mahoteli kila kukicha huko mjini Los Angeles. Gooding alililewa na mama yake na kuhudhuria kwenye mashule tofauti takriban mane: North Hollywood High School, Tustin High School, Apple Valley High School, na John F. Kennedy High School ya mjini Granada Hills huko Los Angeles. Alipata kutumikia kama rais kwenye mashule hayo tofauti matatu. Amekuwa muumini wa dhehebu la Born again akiwa na umri wa miaka takriban 13.[2]
Shughuli za uigizaji
[hariri | hariri chanzo]Filmografia
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Filamu | Uhusika | Maelezo mengine |
---|---|---|---|
1988 | Coming to America | Barber Shop Customer | |
1989 | Judgement | Officer Alvarez | |
Sing | Stanley | ||
1991 | Boyz n the Hood | Tré Styles | |
1992 | Gladiator | Abraham Lincoln Haines | |
A Few Good Men | Cpl. Carl Hammaker | ||
1993 | Daybreak | Torch (Stephen Tolkin) | |
Judgment Night | Mike Peterson | ||
1994 | Lightning Jack | Ben Doyle | |
1995 | Outbreak | Maj. Salt | |
The Tuskegee Airmen | Billy Roberts | ||
Losing Isaiah | Eddie Hughes | ||
1996 | Jerry Maguire | Rod Tidwell | Kashinda Tuzo ya Academy akiwa kama Mwigizaji-Mwandamizi Bora Kateuliwa— Golden Globe |
1997 | As Good as It Gets | Frank Sachs | |
Do Me a Favor | Liquor Store Clerk | ||
1998 | What Dreams Mei Come | Albert Lewis | |
A Murder of Crows | Lawson Russel | Imetayarishwa na Derek Broes | |
1999 | Instinct | Theo Caulder | |
Chill Factor | Arlo | ||
2000 | Men of Honor | BM2/Chief/Senior Chief Carl Brashear | |
2001 | Pearl Harbor | Petty Officer Doris Miller | |
Rat Race | Owen Templeton | ||
Zoolander | Himself | ||
In the Shadows | Draven | ||
2002 | Snow Dogs | Theodore "Ted" Brooks | |
2003 | Boat Trip | Jerry Robinson | |
The Fighting Temptations | Darrin Hill | ||
Radio | James Robert "Radio" Kennedy | ||
2004 | Home on the Range | Buck | voice-over |
2005 | Dirty | Salim Adel | |
Shadowboxer | Mikey | ||
2006 | End Game | Alex Thomas | |
Lightfield's Home Videos | |||
2007 | Norbit | Deion Hughes | |
What Love Is | Tom | ||
Daddy Day Camp | Charlie Hinton | ||
American Gangster | Leroy Barnes | ||
The Land Before Time XIII: The Wisdom of Friends | Loofah | voice-over | |
2008 | Hero Wanted | Liam Case | |
Harold | Cromer | ||
Linewatch | Michael Dixon | ||
The Way of War | David Wolfe | ||
2009 | Gifted Hands: The Ben Carson Story | Ben Carson | TV film |
Lies & Illusions | Isaac | ||
The Devil's Tomb | Mack | ||
Wrong Turn At Tahoe | Joshua | ||
Hardwired[3] | Luke Gibson | ||
2010 | Wrong Side of Town | Clay Freeman | |
Red Tails | TBA |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Gaul, Lou (7 Agosti 2008). "Cuba Gooding Jr. talks 'Daddy Day Camp'". Phillyburbs. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-20. Iliwekwa mnamo 6 Julai 2009.
{{cite web}}
: Italic or bold markup not allowed in:|work=
(help) - ↑ Williams, Kam (15 Agosti 2007). "Cuba Gooding: The Daddy Day Camp Interview with Kam Williams". Kamwilliams. Iliwekwa mnamo 6 Julai 2009.
{{cite web}}
: Italic or bold markup not allowed in:|work=
(help) - ↑ http://www.imdb.com/title/tt1405412/
Viungo vy Nje
[hariri | hariri chanzo]- Cuba Gooding, Jr. at the Internet Movie Database
- Cinema Confidential interview Archived 10 Januari 2018 at the Wayback Machine. (Januari 2002)
- Hollywood.com interview (9 Novemba 2000)
- Jet interview Archived 11 Mei 2005 at the Wayback Machine. (11 Oktoba 1999)
- Ebony interview Archived 7 Novemba 2005 at the Wayback Machine. (Juni 1997)
- JAM! Movies interview (13 Desemba 1996)
- Hanes Backstage Game with Cuba Gooding, Jr. & Michael Jordan Archived 23 Septemba 2009 at the Wayback Machine. (Julai 2007)
- USAToday