Nenda kwa yaliyomo

Tom Cruise

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tom Cruise na Katie Holmes mnamo Juni 2009.
Cruise akiruka kwenye kochi la Oprah.

Tom Cruise (amezaliwa 3 Julai 1962) ni mwigizaji wa filamu kutoka Marekani.

Ndoa ya tatu[hariri | hariri chanzo]

Cruise, aliyekuwa ameshapata talaka mara mbili, aliwahi kumwita Katie Holmes kwa mkutano wa binafsi kwenye ofisi yake. Inasemekana kuwa wawili hawa walianza kupendana baada ya mkutano huu wa masaa manne. [1] Wawili hawa walianza kuonekana mwaka wa 2005 na wana mtoto mmoja aitwaye Suri, aliyezaliwa mnamo 2006.[2][3] Mnamo 27 Aprili 2005, Cruise na Holmes walionekana kwa mara ya kwanza wakiwa pamoja mjini Roma kwenye sherehe ya David di Donatello Awards.

Baada ya mwezi mmoja, Cruise alijulikana kwa kuruka juu ya kochi kwenye kipindi cha Oprah Winfrey akipiga kelele kuwa anampenda Holmes kwa dhati. Baada ya miezi miwili tu ya kujuana, Cruise alimposa Holmes na kuwa mchumba wake katika mkahawa wa Jules Verne iliyo kwenye Eiffel Tower akimvisha pete ya almasi.[4] Mnamo 6 Oktoba 2005, walitangaza kuwa wanatarajia mtoto.[5]

Mnamo 18 Aprili 2006, Holmes alijifungua mtoto wa kike anayeitwa Suri. Mnamo 18 Novemba 2006, miezi saba baada kuzaliwa kwa Suri, wawili hawa walioana mjini Bracciano, Italy.[6] Mwisho wameachana.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. ABC News: "TomKat Expecting TomKitten"
  2. "Can This Be Love?" Archived 5 Januari 2010 at the Wayback Machine. People. 5 Mei 2005. Retrieved 2008-03-01.
  3. "Tom, Katie flying high on romance" USA Today. 5 Mei 2005 Retrieved 2008-04-26.
  4. Melissa Mayntz, LoveToKnow Engagement Rings
  5. Ryan E. Smith. "Baby frenzy begins: Katie Holmes and Tom Cruise are expecting their first child together." Archived 29 Desemba 2020 at the Wayback Machine. The Blade
  6. Soriano, César G. "Mr. and Mrs. TomKat: Inside their fairy-tale wedding", USA Today, 2006-11-20. Retrieved on 2008-02-12.