Casablanca
Casablanca (Kihispania "nyumba nyeupe",tamka kasablanka, ar.| ad-Dār al-Bayḍā’) ni mji mkubwa zaidi nchini Moroko. Ni mji wa bandari uliopo kwenye magharibi ya nchi mwambaoni wa Bahari Atlantiki. Pia ni mju mkubwa kabisa wa nchi za Maghrib na kati ya miji muhimu zaidi kwenye bara la Afrika.
Casablanca ina bandari kubwa ya Moroko[1] ikiwa ni pia kitovu cha benki kubwa za nchi hii. Kufuatana na sensa ya 2012 idadi ya wakazi ilizidi milioni nne katika wilaya yake. Hivyo inatazamiwa kama mji mkuu wa kiuchumi ilhali mji mkuu wa kisiasa ni Rabat.
Jina
[hariri | hariri chanzo]Jina asilia la mahali lilikuwa Anfa kwa lugha ya Kiberber. Wakati wa karne ya 15 Wareno walitwaa eneo hili wakaita mji "Casa Branca" [2]iliyobadilika baadaye kuwa Casa Blanca tangu Wahispania walitawala sehemu hii. Baada ya kuharibika na tetemeko la ardhi mnamo mwaka 1755 na kuondoka kwa Wahispania ni Sultani wa Moroko aliyejenga mji upya na kuuita "A-ddar Al Baidaa" ilhali wenyeji wengi waliendelea kutumia pia jina la Kizungu kwa kuliandika kwa herufi za Kiarabu كازابلانكا (kāzāblānkā) au kwa kifupi "Kaza".
Filamu
[hariri | hariri chanzo]Casablanca ni jina la filamu iliyopigwa mwaka 1942 huko Hollywood. Inasimulia hadithi ya wakimbizi kutoka nchi za Ulaya wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia na utawala wa ufashisti wa Kijerumani katika nchi nyingi waliokutana mjini Casablanca wakitumaini kupata njia kukimbilia Ureno iliyokuwa bado nchi huru. Waigizaji wakuu walikuwa Humphrey Bogart na Ingrid Bergman na filamu ikapata tuzo tatu za Academy Awards.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Discovering Casablanca". Africa-ata.org. Iliwekwa mnamo 17 Aprili 2011.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Nyumba nyeupe" kwa Kireno