Carolyne Ekyarisiima

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Carolyne Ekyarisiima (amezaliwa 20 Juni 1986) ni mjasiriamali, mwanasayansi katika nyanja ya kompyuta na mwasisi wa shirika lisilokuwa la kiserikali la apps and girls lenye malengo ya kuongeza idadi ya wanawake kutumia teknohama kutengeneza miradi ya kusaidia jamii zao[1].

Kupitia taasisi yake ya apps and girls anatoa semina na mafunzo mbalimbali kwa wanafunzi waliopo katika shule za sekondari, pia ameanzisha klabu za kujifunza mambo ya teknolojia katika shule, ambapo kupitia klabu hizi wanafunzi hukutana kujifunza na kushirikishana mambo mbalimbali yahusuyo teknohama.

Wasichana wameweza kujifunza namna ya kutengeneza tovuti, programu za kwenye simujanja na pia namna ya kuweza kujieleza mbele ya wafadhili wanapokuwa wanataka kuomba pesa kwa ajili ya kuendeleza programu zao.[2]

Maisha yake[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa wilayani Bushenyi nchini Uganda katika familia ya watoto saba yeye akiwa wa tano.

Alitumia muda wake mwingi kuchunga ng’ombe, lakini pia aliweza kupata muda wa kwenda shule kwa kuwa baba yake alikuwa mwalimu wa Shule ya msingi na alithamini sana elimu.[3]

Elimu yake[hariri | hariri chanzo]

Carolyne ana shahada ya sayansi ya kompyuta na shahada ya uzamili ya mifumo ya habari (Information Systems) kutoka katika chuo cha kimataifa cha Kampala.[4]

Tuzo Mbalimbali[hariri | hariri chanzo]

Aliwahi kujishindia pesa kiasi cha dola 25000, zilizokuwa zikitolewa na Tigo kwa ajili ya kudhamini watu wanaojihusisha na kuleta mabadiliko ndani ya jamii kupitia teknolojia.[5] aliweza kutajwa kama mmoja wa wavumbuzi bora 20 wa mwaka,waliokuwa wakiwania tuzo hiyo(innovator of the year award)inayo tolewa na AIDF [6]

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Carolyne Ekyarisiima kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]