Apps and Girls
Aina | Taasisi Isiyo Ya Kiserikali |
---|---|
Ilipoanzishwa | 27/03/2014 |
Waanzishi | Carolyne Ekyarisiima, Wilhelm Caspar Oddo |
Makao Makuu | , Tanzania
Dar Es Salaam, Tanzania Dar Es Salaam, Tanzania |
Tovuti | https://www.appsandgirls.com/ |
Apps and Girls ni asasi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa na Carolyne Ekyarisiima na kusajiliwa na Wizara ya Jinsia, Wanawake na Watoto nchini Tanzania mwaka 2014. Ni taasisi yenye kuwasaidia mabinti na wanawake wadogo katika nyanja ya habari na mawasiliano ambapo inafanya kazi kwa kuwafundisha wanafunzi namna ya kutengeneza programu za kompyuta na biashara, pia mambo ya kutengeneza roboti.
Zaidi ya hayo taasisi hiyo inafanya kazi ya kuwainua mabinti walioshindwa kuendelea na shule katika viwango tofauti kwa kuwaingiza kwenye Mradi wa Jovia ambapo mabinti hao wanapewa mafunzo mbalimbali yenye kuongeza nafasi zao za kupata ajira katika sekta ya habari na mawasiliano; mafunzo hayo pia huwasaidia kuanzisha biashara zao ama kukuza biashara walizonazo.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Carolyne Ekyarisiima alikuwa ni Mkufunzi msaidizi katika chuo kikuu cha Kampala International University katika tawi la Dar es salaam lililoko nchini Tanzania kuanzia mwaka 2009 mwishoni. Akiwa Mkufunzi msaidizi, alifundisha masomo ya Computer Science ikiwamo Programming katika lugha ya C, Java na PHP.[1]
Kufundisha masomo hayo kukamfanya atambue gepu lililopo katika darasa lake ambalo lilikuwa na wanafunzi wengi wakiume huku mabinti wakiwa wachache. Ndipo mwaka 2013 akaandaa mafunzo ya wazi kwa Wanawake walioko katika ajira na walioko mavyuoni kuja pamoja na kujadili mambo yanayo husu Teknolojia na kutoa mafunzo ya Kutengeneza tovuti kwa kutumia Joomla.
Programu za Apps and Girls
[hariri | hariri chanzo]- Coding Clubs: Apps and Girls ni taasisi ya kwanza nchini Tanzania kufundisha "Computer Programming" kwa wanafunzi wa secondary hususani mabinti Umri miaka 12 na Kuendelea. Ni taasisi iliyo jikita katika matumizi ya Tehama kwa kuwafanya vijana wadogo, hususani mabinti, kuweza fanya mambo makubwa ambayo yalikuwa yakifanywa na watu wakubwa katika ulimwengu wa TEHAMA na biashara. Njia kubwa iliyotumiwa na Carolyne na taasisi yake ya Apps and Girls ni kupita katika shule binafsi na za serikali za sekondari, wakianza na shule za jijini Dar es Salaam na baadae mikoa mingine[2]. Lengo la mwanzilishi wa taasisi hii, Carolyne Ekyarisiima, lilifanikiwa pakubwa hasa baada ya kuwaandaa mabinti wadogo kama Modesta Joseph, mwanzilishi wa Tovuti ya "Our Cries" au "OVAH[3]". Huyu ni mmoja wa mabinti ambao walianza kufanya mambo makubwa katika jamii zao wakiwa na umri mdogo. Kupitia taasisi yake ya Ovah aliweza kuanzisha mfumo wa kidijitali uliotumika kuwasaidia wanafunzi pale wanaponyanyaswa, lengo likiwa ni kupunguza manyanyaso katika vyombo vya usafiri kwa wanafunzi, hususani "daladala".[4]
Wanafunzi wengine walio nufaika na Mradi huu ni Pamoja na Winnie Msamba[5], Asha Abbas[6], Fatuma Abbas[7], Necta Richald[8], Julieth Sewava[9], Hyasinta Luhanga[10], Balbina Gulam[11], Queen Mtega[12] Na Lisa Jones[13]. Kiujumla Coding Clubs hizi zipo Tanzania nzima kwa kushirikiana na Makampuni ya Tigo na Wadau wengine, Mpaka mwaka 2023 Jumla ya wanafunzi walio fanikiwa pitia katika mradi huu ni zaidi ya 100,000 huku asilimia 60 ya wanafunzi wakichagua kuendelea na masomo ya Sayansi (STEM). - Girls Entreprenuership Summit: Huu ni Mkutano mkubwa wa kiteknolojia ambao hukutanisha mabinti na wasichana wadogo walioko mashuleni (Shule za serikali na shule Binafsi) lengo likiwa ni kuwakutanisha na wadau kwenye ulimwengu wa Teknolojia, Mainjinia, Wanasayansi na wafanya biashara[14]. Mkutano huu ni maalumu kwa wanafunzi wa kike ingawa kutokana na mvuto wake wanafunzi wa kiume pia hujikuta wakishiriki. Mradi huu ulianza mwaka 2017 na umekuwa ukifadhiriwa na Ubalozi wa Marekani na wadau wengine kama Tigo Tanzania. Wanafunzi huanza miezi sita nyuma ambapo wakiwa mashuleni kwao huanza kufundishwa Biashara na Uandishi wa codes za kompyuta kisha hukusanya mawazo yao na kushiriki katika mashindano ambapo Vitengo mbali mbali huibua washindi katika mashindano hayo na washindi huendeleza miradi yao na kufanikisha kuwa Biashara kamili au Taasisi zenye kutatua Changamoto katika Jamii.[15]
- Jovia Program: Mradi huu ni maalumu kwa wanafunzi ambao kutokana na changamoto kadhaa za maisha hawakuweza fanikiwa pata nafasi ya kumalizia masomo yao katika kiwango chochote kile kuanzia secondari mpaka chuo kikuu. Hii inatokana na kuongezeka kwa mabinto wasio na ajira rasmi ambapo kisababishi kikubwa cha wao kukosa hiozi ajira ni aidha hawana maarifa ya kutosha ama hawana elimu kabisa na kukosa sifa za kuajirika. Jovia inarudisha nuru na matumaini katika nafsi zao. Carolyne anasema "Sababu kuu ya kuianzisha Program hii ni namna ambavyo mama yangu alipenda sana elimu wakati wake, ila kutokana na sababu kadhaa hakuweza fanikisha ndoto zake kikamilifu. Nikaianzisha Program hii na kuipa Jina lake kama kumbukumbu". Tangu kuanzishwa kwake mradi huu umegusa mabinti na wanawake wengi, Mfano; Aslatu Nguku[16] Mwanzilishi wa mradi wa Mama Health mradi ambao ulianzishwa mara baada ya kujiunga na Jovia na leo umekuwa ni mradi mkubwa ukiwasaidia wanawake katika chanhamoto zao nyakati za kujifungua. Mradi huu wa mama health umefanikiwa kushikwa mkono na mashirika na taasisi kubwa ndani ya Tanzania na hivyo kuokoa maisha ya mama na mtoto. Mradi wa Jovia umekuwa ni mradi wenye mafanikio makubwa na kupelekea kupata tuzo kadhaa za Kimataifa Kama WSIS Prize Champion katika mambo ya kuwajengea watu uwezo iliyo andaliwa na shilika la kimataifa la ITU (International Telecommunication Union) ya mwaka 2020[17] na mwaka 2023 mradi huo ukawa ni mradi ulio shinda katika tuzo hizo kidunia kwenye kategoria ya ajira "Global Winner in E-Employment".[18]
- ADA Lace Program: Ni mradi maalumu kwa ajili ya wanafunzi wa Chuo kikuu ambao wamemaliza chuo na wapo mtaani pasipo kuwa na ajira aidha kutokana na ukosefu wa ajira ama kutokana na kuwa na maarifa lakini maarifa yao hayana mashiko mbele ya macho ya mwajiri. Mradi huu hujikita katika kutoa mafunzo ya Akili bandia "Artificial Intelligence" na pia mafunzo ya kidijitali ambayo soko la ajira lina hitaji kwa wakati huo. Mradi huu ulipo anza ulikuwa unasapotiwa na program ya SAIS[19].
- Robotics: Haya ni mafunzo ambayo hutolewa kwa wanafunzi wa kike na wakiume wenye mapenzi na teknolojia. Mafunzo haya huenda sambamba na ufundishaji wa kutengeneza program za kwenye Computer. Mwaka 2017 Taasisi ya Apps and Girls ikishirikiana na IETWC na FIRST Global waliweza toa mafunzo kwa wanafunzi na kisha kushiriki katika mashindano ya Dunia yaliyo fanyika nchini Marekani huku Tanzania Ikishika namba 92 katika nchi 157 zilizo shiriki. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa wanafunzi hawa kushiriki mashindano makubwa kama hayo kidunia, na ukawa ni mwangaza bora kwao. Walio Shiriki ni pamoja na Lisa Jones Kutoka Jangwani Secondary School (Msichana), Modesta Joseph Kutoka Kisutu Secondary School (Msichana), Kokubanza Timanywa[20] Kutoka Jangwani Secondary School (Msichana), Godbright Nixon[21] kutoka Azania Secondary School (Mvulana), Raymond Benedict[22] kutoka Jamuhuri Secondary School (Mvulana), Sangali Tindi kutoka Feza Secondary School na Francis Mwasolya kutoka Kibasila Secondary School (Mvulana). Apps and Girls Imekuwa ikishirimi mashindano hayo kila Mwaka ambapo Mwaka 2018 mashindano hayo yalifanyika Nchini Mexico na Tanzania ikawakilishwa na wanafunzi wawili ambao ni Zainabu Omari (Msichana) kutoka Benjamini High School na Anatory Anjelo (Mvulana) Kutoka Padre Pio Secondary School. [23] Mwaka 2019 Wanafunzi wa Apps and Girls Walishiriki mashindano hayo yaliyo fanyika nchini Dubai. Ushiriki huu ulihusisha wanafunzi Doreen Michael kutoka Jangwani Secondary School, Julieth Sewava kutoka Jangwani Secondary School, Hajra Honero (Msichana) kutoka Korogwe Girls Secondary School. Kutokana na kuzuka kwa janga la CORONA, Mashindano haya yalisimamishwa na yakaja kurudi mwaka 2022 ambapo Tanzania ikawakilishwa na wanafunzi wa apps and Girls ambao ni Beldi Zikudia[24] kutoka Mugabe Secondary School, Maria Johnbosco Mtega (Msichana) kutoka St Theresa Secondary School, Joseph Joseph Msabila (Mvulana) , Hellen na Amezia.[25] Ushiriki wa mwaka 2022 ulileta faraja kubwa baada ya Team Tanzania kupata medali ya Madini ya Fedha na ushindi huu ukawakutanisha wanafunzi hawa na Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano Mheshimiwa Nape Nnauye na Baadaye Waziri mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa ambaye aliwapa Mualiko maalumu vijana hawa wa kwenda Bungeni Dodoma na kuweza pewa heshima yao na Wabunge na Mawaziri wote huku wakipokea salamu za pongezi kutoka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.[25]
Apps and Girls Uganda
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 2019 Taasisi ya Apps and Girls iliona haja ya kuanzisha Mradi unao fanana na huu uliopo Tanzania katika nchi za jirani hasa kutiokana na kupokea maombi mengi kutoka kwa mashule na wazazi wenye kutamani watoto wao kupata nafasi ya kujifunza na kuweza fanya mambo mazuri na makubwa. Apps and Girls ikasajiriwa nchini Uganda ikiwa na jina Hilo hilo.
Hivyo Apps and Girls Uganda ni taasisi iliyo sajiriwa nchini Uganda ikifanya kazi sawa sawa na zinazo fanywa nchini Tanzania. Ili kuweza wafikiwa wanafunzi kwa haraka Apps and Girls ikaanza kwa kuandaa "BootCamp" Mafunzo bora ya muda mfupi yenye kukutanisha watu wengi kwa wakati mmoja. Hivyo Cohort ya Kwanza ilipewa nafasi ya kujifunza Mafunzo ya kutengeneza roboti ya First Global Challenge[26] , na kuweza shiriki katika mashindano ya Robotics nchini Dubai. Ushiriki wa Team hii nchini Dubai ukaipa ushindi na hivyo kuondoka na Medali ya Fedha.[27]
Mwaka 2022 Apps and Girls iliweza fanya Boot Camp kwa wanafunzi mbali mbali wa shule za secondary ikisaidiwa na The Rockefeller Foundation na kuweza wafikia mabinti wengi. Team ikashiriki Mashindano ya Robotics nchini Switzland na Kuibuka na Ushindi wa tuzo Mbili moja ikihusisha team nzima na nyingine ikimhusisha Akampa Mitina ambaye alishinda tuzo ya Temasek Women in STEM Award.
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]- Social Inclusion Award (2019) By Women in Tech[28]
- WSIS Prize (2020) Champion in Capacity Building by ITU [17]
- 1st runners up for the ATU Africa Innovation challenge (2021) By African Telecommunication union and ITU[29]
- Overall winner of the ICT awards (2021) By the Tanzania ICT commission
- Best ICT Incubator of the year (2021) By the Tanzania ICT commission
- Global Winner in E-Employment (2023) By WSIS[18]
- Entrepreneurship Education Program Award (2023) By ASEB UNSUNG HERO[30]
Hadithi za mafanikio
[hariri | hariri chanzo]- Wanafunzi kupata fursa ya kufahamiana na watu
- Wanafunzi kupata fursa ya kujiendeleza kimasomo
- Wanafunzi kupata fedha za kuendesha miradi
- Wanafunzi kuanzisha Biashara na Miradi mikubwa yenye Mafanikio
Ushirikiano
[hariri | hariri chanzo]- US Embassy
- Africa Code Week
- UNICEF
- TIGO
- Wizara ya Elimu
- W4
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.w4.org/en/wowwire/apps-and-girls-changing-the-world/
- ↑ Editorial Team (2022-04-29). "Tigo Helps 'Apps and Girls' Launch the Third Phase of the Girls & Women Empowerment 2022 Project". TechAfrica News (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-02-05.
- ↑ "MODESTA JOSEPH". We Are Family Foundation (kwa American English). 2021-07-02. Iliwekwa mnamo 2024-02-05.
- ↑ "Students use tech to fight abuse in daladalas | The Citizen". www.thecitizen.co.tz. Iliwekwa mnamo 2024-02-05.
- ↑ Abroad, Actuality (2016-09-22), Girls Like Us, iliwekwa mnamo 2024-02-06
- ↑ "25 under 25 Awardees". Internet Society (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-02-06.
- ↑ Bertelli, Michele (2019-03-16), "Tanzania y el tirón de la educación sexual 'online'", El País (kwa Kihispania), ISSN 1134-6582, iliwekwa mnamo 2024-02-06
- ↑ Mtanzania Digital (2016-07-15). "NECTA RICHARD: Nataka kuwa mhandisi kuisaidia nchi yangu". Mtanzania (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-02-06.
- ↑ Mwandishi Wetu (2021-10-05). "Wadau waiangukia Serikali ajira za utotoni, wasichana kuachwa nyuma kidigitali" (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-02-06. Iliwekwa mnamo 2024-02-06.
- ↑ Abdi Latif Dahir (2018-02-24). "How Tanzania is betting on coding to help close the gender gap in its tech sector". Quartz (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-02-06.
- ↑ adreci (2020-03-30). "Digital Learning and Livelihoods of Domestic Workers in Tanzania". ADRECI - Africa Development Resources and Capacities Institute (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2024-02-06.
- ↑ "Queen: Msichana aliyebuni tovuti kuwasaidia vijana mafundi". Mwananchi (kwa Kiingereza). 2021-03-15. Iliwekwa mnamo 2024-02-06.
- ↑ FIRST Global (2018-06-11). "Team Tanzania 2018". FIRST Global (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-02-06.
- ↑ https://www.ippmedia.com/en/business/be-innovative-and-technology-savvy-girls-challenged#google_vignette
- ↑ "Bridging the tech gender gap in TZ". The Citizen (kwa Kiingereza). 2021-04-01. Iliwekwa mnamo 2024-02-06.
- ↑ "AWE yawapatia mafunzo wanawake kuwa Wajasriamali bora Afrika Mashariki". Voice of America. 2023-07-12. Iliwekwa mnamo 2024-02-06.
- ↑ 17.0 17.1 "Champion Projects — WSIS Prizes 2020". www.itu.int. Iliwekwa mnamo 2024-02-05.
- ↑ 18.0 18.1 "Nominated Projects — WSIS Prizes 2023". www.itu.int. Iliwekwa mnamo 2024-02-05.
- ↑ "SAIS - Southern Africa Innovation Support". saisprogramme.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-02-06. Iliwekwa mnamo 2024-02-06.
{{cite web}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - ↑ "Connecting Students to Textbooks | Data Collaboratives for Local Impact" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-02-06.
- ↑ "Robots are set to take Africa's manufacturing jobs even before it has enough". Quartz (kwa Kiingereza). 2017-07-26. Iliwekwa mnamo 2024-02-06.
- ↑ Michuzi Blog. "Stella Manyanya akabidhi bendera kwa wanafuunzi watakaoiwakilisha nchi katika mashindano ya first lbal Robotic Challenges nchini Marekani". MICHUZI BLOG. Iliwekwa mnamo 2024-02-06.
- ↑ FIRST Global (2018-06-11). "Team Tanzania 2018". FIRST Global (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-02-06.
- ↑ #WiDSAFRICA2022 Testimonial: Beldi Zikudia, iliwekwa mnamo 2024-02-06
- ↑ 25.0 25.1 "Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Awaalika Bungeni Wanafunzi Walioiwakilisha Nchi Uswizi Kuunda Roboti". Global Publishers (kwa American English). 2023-02-02. Iliwekwa mnamo 2024-02-06.
- ↑ "FIRST Global Challenge", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2023-12-04, iliwekwa mnamo 2024-02-06
- ↑ FIRST Global (2019-07-27). "Team Uganda 2019 🇺🇬". FIRST Global (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-02-06.
- ↑ "Winners". Women in Tech Challenge (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-02-05. Iliwekwa mnamo 2024-02-05.
- ↑ "Tunisian, Tanzanian and Zambian Initiatives win ATU's Africa-wide Competition Building Youth ICT Innovation Ecosystems". African Telecommunications Union (kwa American English). 2021-10-14. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-02-05. Iliwekwa mnamo 2024-02-05.
{{cite web}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - ↑ "Awards - ASEB Summit" (kwa American English). 2022-02-08. Iliwekwa mnamo 2024-02-05.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- https://pdetic.wixsite.com/nomadontheroad/single-post/2014/11/21/apps-girls-empowering-tanzanian-girls-with-ict
- https://dailynews.co.tz/young-women-project-wins-prestigious-award/
- https://womenintech-challenge.com/apps-and-girls/ Ilihifadhiwa 28 Februari 2022 kwenye Wayback Machine.
- https://www.w4.org/en/wowwire/apps-and-girls-changing-the-world/
- https://www.axian-telecom.com/cirdowee/2023/03/Girls-Young-Women-Empowerment-JOVIA-Program-Win-WSIS-2023-Geneva-V3-002.pdf
- https://www.ippmedia.com/en/business/tigo-apps-and-girls-partnership-develop-tech-savvy-girls
- https://westafricanbusinessjournal.com/2017/05/18/1-million-african-childrens-lives-improved-local-social-entrepreneurs-supported-reach-change-africa/ Ilihifadhiwa 5 Februari 2024 kwenye Wayback Machine.
- https://www.youtube.com/watch?v=XRVKiGGuXuU
- https://www.itu.int/en/ITU-D/Digital-Inclusion/Women-and-Girls/Girls-in-ICT-Portal/Pages/events/2016/Africa/Tanzania-2016-1.aspx
- https://swahilionlineblogg.blogspot.com/2017/04/vijana-wa-kitanzania-wanaotengeneza.html
- https://cms.nukta.co.tz/msichana-wa-miaka-19-aibuka-na-suluhisho-la-fundipopote/
- https://www.matukiodaimamedia.co.tz/2022/10/washiriki-wa-first-global-robotics.html
- https://www.youtube.com/watch?v=deO5ECKSVsI
- https://www.aa.com.tr/en/africa/girl-coders-aim-to-bridge-tech-gender-gap-in-tanzania/2021605
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |