Nenda kwa yaliyomo

Modesta Joseph Msabila

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Modesta Joseph Msabila
Amezaliwa 12 Agosti 1999 (1999-08-12) (umri 25)
Dar es Salaam
Nchi Tanzania
Makazi Rwanda
Anafahamika kwa Mwanzilishi wa tovuti ya Our Cries na Taasisi ya Ovah
Miaka ya kazi 2014 Mpaka sasa
Elimu Kisutu Secondary School - 2014 -2017

Apps and Girls (Tech Entrepreneurship) 2015 - 2020
African Leadership Academy (ALA) 2018 - 2020
African Leadership University (ALU) -2021

Asasi Ovah (Our Cries Against Gander Based Violence and Harassment)
Mwanachama bodi ya Apps and Girls
Tuzo Innovator of the Year
Tovuti https://ovah.or.tz


Modesta Joseph Msabila (alizaliwa 12 Agosti 1999 (1999-08-12) (umri 25)) ni mwanaharakati, mjasiriamali Jamii ambaye anatumia teknolojia ya habari na mawasiliano katika kuisaidia jamii yake nchini Tanzania. Ni mwanzilishi wa tovuti iliyoitwa "Our Cries[1]" aliyoianzisha akiwa na umri wa miaka 16 tu na kuweza shinda tuzo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

Modesta Joseph Msabila ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto wawili ambapo baba yake mzazi anaitwa Joseph Msabila, na mama yake anaitwa Maria Ntaga, huku mdogo wake akiitwa Joseph Joseph Msabila.

Kukua kwake katika maisha ya kawaida kulimfanya ayajue maisha ya mtanzania wa chini hasa kutokana na kusoma katika shule za serikali maarufu kama Kayumba. Katika kukua kwake Modesta hakuwa mtu wa kuchangamana sana na wageni, ingawa yeye mwenyewe anasema mara kadhaa alitamani kujichanganya na watu lakini alijikuta nafsi ikimsukuma kujiweka mbali na kuendelea na hamsini zake.[2]

Kuanzishwa kwa Club ya Computer shuleni kwao chini ya uangalizi wa taasisi ya Apps and Girls ambayo ilipelekea Kuletwa kwa Computer za Kisasa shuleni kwao Kisutu na kukarabatiwa kwa Maabara ya Computer na Kampuni ya MIC Tanzania Limited (Tigo) kukamfanya atamani kufahamu kila linalo wezekana katika ulimwengu huo mpya wa TEHAMA.

Elimu yake

[hariri | hariri chanzo]

Modesta alipata elimu yake ya awali katika shule ya Kigilagila iliyoko Kiwalani jijini Dar es salaam mwaka 2008 mpaka mwaka 2015 alipo hitimu darasa la saba. Kigilagila ni shule ya serikali iliyo karibu na uwanja wa kimataifa wa mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Alisoma mpaka darasa la saba na kujiunga na shule ya upili baada ya kufaulu vizuri masomo hayo.

Alijiunga na shule ya Upili (Sekondari) mwaka 2016 mara baada ya kufaulu vyema masomo ya awali na kuhitimu mwaka 2019 ambapo pia alifaulu vyema na kuchaguliwa kwenda Kidato cha tano. 

Mwaka 2020 Modesta akachaguiwa kwenda kusoma Masomo ya advance nchini Africa Kusini katika Shule maarufu duniani kwa kuwaandaa vijana kuwa wafanyabiashara, wanasayansi, wanasanaa na viongozi wakubwa. Ni shule maarufu yenye mafanikio makubwa.

Mwaka 2022 Modesta akajiunga na Chuo kikuu cha ALU kilichopo nchini Rwanda kujiendeleza na masomo ya juu.

Harakati

[hariri | hariri chanzo]

Ovah ni moja kati ya taasisi zenye kupigania haki za mabinti nchini Tanzania. Chini ya uongozi wa mwanzilishi ambaye ni Modesta, Taasisi hii imekuwa ikifanya mambo mengi katika jamii hususani kutoa elimu juu ya mambo ya haki za binadamu kwa wanafunzi wa jinsia zote huku kipaumbele kikiwa ni kwa wanafunzi na watoto wadogo.[3]

Wakati wa kuanza kwake, Modesta akiwa na Umri wa miaka 16 aliweza kwenda LATRA (zamani SUMATRA) ambayo ni Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini na kuonana na mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo ambaye alishangazwa na ujasiri wake na bila kipingamizi bodi hiyo iliweza kufanya naye kazi katika shughuli mbalimbali huku ikiutumia mfumo wa Our Cries kama sehemu mojawapo ya kupata taarifa za madereva wakorofi. Modesta hakuishia hapo, aliweza pia kukutana na Kaimu Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Trafiki Tanzania, SACP Fortunatus Musilimu ambaye naye alishangazwa na umri wake na namna alivyo na nia ya kuipambania nchi yake. Hivyo Modesta kupitia mfumo wake wa Our Cries akawa anafanya kazi na idara hiyo katika kutoa elimu na semina kwa wanafunzi kuhusu matumizi salama ya barabara huku ripoti za unyanyasaji katika vyombo vya usalama zikitokea basi zinapelekwa moja kwa moja SUMATRA na Idara ya usalama barabarani.

Haki za Binadamu

[hariri | hariri chanzo]

Mfumo wa OurCries uliotengenezwa na Modesta Joseph akiwa bado ana miaka 16 ulitumika na Taasisi ya Human watch kama moja ya sehemu ya kutazama taarifa za unyanyasaji kwa wanafunzi unaofanywa na wanajamii katika nyanja mbalimbali. [4]

Tuzo na Teuzi Mbalimbali

[hariri | hariri chanzo]
  1. Global teen leaders of 2017 By WE ARE FAMILY FOUNDATION [5]
  2. Tech Leader AWARD of 2014 By Apps and Girls
  3. Innovation Fund grant of 2014 By TANZICT [6]
  4. SLUSH Attendee in Finland (2014) [7]
  5. Anti Gender based Champion By Wildaf (2022)
  6. Tanzania 100 Sheroes By Launchpad (2022)
  1. "Students use tech to fight abuse in daladalas | The Citizen". www.thecitizen.co.tz. Iliwekwa mnamo 2024-02-05.
  2. Letter from Africa: The teenager fighting school bus sex pests (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2018-04-21, iliwekwa mnamo 2024-02-05
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-02-14. Iliwekwa mnamo 2024-02-14.
  4. https://www.hrw.org/sites/default/files/report_pdf/tanzania0217_insert_lowres_spreads.pdf
  5. "MODESTA MSABILA". We Are Family Foundation (kwa American English). 2021-06-13. Iliwekwa mnamo 2024-02-05.
  6. https://tanzict.files.wordpress.com/2016/12/tanzict_end_publication.pdf
  7. "Innovation programme turns young Tanzanians into entrepreneurs". Finland abroad: Tanzania (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-02-05.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  1. https://www.the-star.co.ke/news/2018-04-22-the-tanzanian-teenager-fighting-school-bus-sex-pests/
  2. https://gettotext.com/modesta-joseph-she-makes-girls-stand-up-against-sexual-harassment/
  3. https://www.hindustantimes.com/delhi-news/must-protect-teenage-girls-against-daily-harassment/story-wogribxh7p7g6b13PMpB8N.html
  4. https://changing-transport.org/why-aspire-to-buy-more-cars/
  5. https://www.bbc.com/gahuza/amakuru-43885176
  6. https://www.brigitte.de/aktuell/gesellschaft/modesta-joseph--sie-macht-maedchen-gegen-sexuelle-belaestigung-stark-13143376.html
  7. https://www.fr.de/zukunft/storys/technologie/die-jungen-coding-queens-von-silicon-dar-91022030.html
  8. https://thanhnien.vn/co-gai-kien-cuong-chong-nan-yeu-rau-xanh-tren-xe-buyt-185751873.htm
  9. https://www.hrw.org/sites/default/files/report_pdf/tanzania0217_insert_lowres_spreads.pdf
  10. https://www.ndr.de/nachrichten/info/podcasts/Der-Wandel-ist-Weiblich-5-Tansania,derwandelistweiblich158.html
  11. https://www.kenyapaediatric.org/wp-content/uploads/2018/05/Global-Adolescent-Health-Prof.-Susan-Sawyer.pdf
  12. https://news.trust.org/item/20160212140343-adjhd
  13. https://gogetfunding.com/modesta-with-launchx-mit-summer-program/