Carlos Ruckauf

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Naibu Rais wa Argentina wa 31
Muda alipokuwa ofisini:
8 Julai 1995 – 10 Desemba 1999
Rais wake: Carlos Saúl Menem
Kabla yake: Eduardo Duhalde
Baada yake: Carlos Álvarez
Gavana wa Buenos Aires
1999-2002
Kabla yake : Eduardo Duhalde
Baada yake: Felipe Solá
Alizaliwa: 10 Julai 1944(1944-07-10) Ramos Mejía

Carlos Federico Ruckauf (alizaliwa 10 Julai 1944) ni mwanasiasa wa Kiperonisti wa nchi ya Argentina. Yeye ni mwanachama wa Chama cha Justicialista.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Yeye alikuwa Waziri wa Kazi katika serikali ya Isabel Perón kabla ya mapinduzi ya kijeshi ya Machi 1976, alitia saini amri ya 261/75 iliyoamrisha "kuangamizwa kwa watu" na kuanzisha kilichoitwa "Vita Vichafu". Baada ya mwaka wa 1983, uanzishaji tena wa serikali wa raia, Carlos alikuwa Waziri wa Ndani kisha akawa naibu wa rais wa Argentina mnamo Julai 1995 katika serikali ya Carlos Menem na akabaki katika ofisi hiyo hadi Desemba 1999, serikali ya Menem ilipotoka uongozini. Katika uchaguzi wa 1999, alichaguliwa kuwa gavana wa jimbo la Buenos Aires.

Ruckauf alitoka cheo hicho katikati ya migogoro ya kisiasa ya Argentina mnamo Desemba 2001 ili kujiunga na serikali ya Eduardo Duhalde. Akawa Waziri wa Shughuli za Kigeni na akabaki katika cheo hicho hadi 25 Mei 2003, serikali ya Duhalde ilipotoka uongozini.

Baadaye katika mwaka wa 2003, Ruckauf aliteuliwa kuwa mwakilishi wa Mkoa wa Buenos Aires katika Chemba ya Argentina ya Manaibu. Alikuwa katika upande wa Kiperonisti uliopinga serikali ya Nestor Kirchner hadi alipotoka Congress katika mwaka wa 2007.

Congress ya Argentina katika jimbo la Buenos Aires ambalo Carlos alikuwa gavana tangu 1999 hadi 2002.

Kabla ya na katika miaka ya 1980[hariri | hariri chanzo]

Carlos Ruckauf alianza kufanya kazi kama katibu. Uhusiano wake na Lorenzo Miguel, kiongozi wa Unión Obrera Metalúrgica(muungano wa wafanyikazi wa kuunda vitu vya chuma) ulimsaidia kuwa Waziri wa Leba wa Rais Isabel Peron mnamo Julai 1975,kazi aliyofanya mpaka mapinduzi ya Machi 1976 yalipofanyika. Carlos aliweza kuponea kutiwa nguvuni,si kama Waperonisti wengine walioshikwa na serikali mpya ya kijeshi. Inasemekana kuwa aliokolewa na Mwanajeshi Eduardo Massera,yeye mwenyewe akiwa Mperonisti, kwa kupitia afisa wa Polisi, Ramón Ramírez.

Tangu miaka ya 1980 mpaka leo[hariri | hariri chanzo]

Carlos Ruckauf akawa rais wa Chama cha Justicialista katika jiji kuu la Buenos Aires katika mwaka wa 1983, chini ya Raúl Alfonsín. Baada ya kuwa na cheo cha naibu,alipandishwa hadhi na kuwa balozi spesheli wa Argentina nchini Uitalia,Malta na FAO(1989-91), Waziri wa Mambo ya Ndani (1993) kisha makamu wa rais wa Argentina (1995) chini ya Carlos Menem, jukumu lake lilitiwa mashakani na familia za waathiriwa wa Mlipuko wa 1995 wa AMIA.

Alichaguliwa kuwa gavana wa Jimbo la Buenos Aires katika mwaka wa 1999,akatoa Patacón, vifungo maalum vilivytolewa katika mwaka wa 2001 katika jimbo hilo ili kukabiliana na uhaba wa peso za Argentina(hela ya Kiargentina).

Ameshtakiwa kwa "kupotea" kwa wafanyikazi 14 wa Mercedes Benz katika mwaka wa 1975.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Un documento prueba que Ruckauf pedía que se reprimiera ilegalmente a trabajadores, La Fogata
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Carlos Ruckauf kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.