Nenda kwa yaliyomo

Carlos Álvarez

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Makamu wa Rais wa 32 wa Argentina
Muda alipokuwa ofisini
10 Desemba 1999 – 6 Oktoba 2000
Rais wake: Fernando De la Rua
Kabla yake: Carlos Ruckauf
Baada yake: Daniel Scioli
Alizaliwa: 26 Desemba 1948 (1948-12-26) (umri wa miaka 61)
Alipozaliwa: Buenos Aires, Argentina
Uzalendo: Argentina
Shahada: Digrii ya Historia

Carlos Alvarez (makamu wa rais)

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Carlos Alberto "Chacho" Alvarez (alizaliwa tarehe 26 Desemba 1948 katika Buenos Aires) ni mwanasiasa wa Argentina; yeye alikuwa Makamu wa Rais wa Argentina katika sehemu ya utawala wa Rais Fernando de la Rua, na sasa anaongoza Mercosur Sekretarieti.

Carlos Álvarez

Alvarez alimaliza shahada yake ya digrii katika historia katika Chuo Kikuu cha Buenos Aires. Yeye alikuwa mtu wa kuchunguza kazi iliyofanywa na Tume ya Uchumi wa Majimbo ya Seneti ya Taifa kutoka miaka ya 1983 hadi miaka ya 1989. Mwaka uo,wa 1989, alichaguliwa kama Naibu wa Taifa wa Chama cha Justicialista lakini akatoka chama hicho muda mfupi baadaye kwa sababu ya migogoro na Rais Carlos Menem. Akianzisha kikundi kilicho huru kilichoitwa The Group of the Eight (kikundi cha Wanane).

Katika mwaka wa 1991,Alvarez alijiunga na kundi la wanasiasa wa vyama mbalimbali za maendeleo, vilevile wanachama wa zamani wa Justicialista, ili kuunda chama cha umoja wa Frente Grande. Yeye alichaguliwa kuwa mwakilshi katika Congress katika muda wa 1993-1997, na vilevile kuwa mwanachama wa Mkutano wa Katiba uliofanya mabadiliko katika katiba katika mwaka wa 1994, bado akiwa mwanachama wa Frente Grande. Katika mwaka wa 1994 alichukua jukumu fulani katika uumbaji wa chama cha FrePaSo. Alikuwa mgombea wa Makamu wa Rais akiwa na mwenzake José Octavio Bordón,aliyegombea urais, wakapata nafasi ya pili katika uchaguzi wa rais wa 1995.

Katika mwaka wa 1997,FrePaSo ilijiunga na muungano wa Unión Civica Radical ili kuumba Muungano wa Kazi,Haki na Elimu(inajulikana sana kama Alianza). Alvarez alichaguliwa tena katika kiti cha Naibu wa Taifa katika Chemba ya Manaibu, wakati huu akichaguliwa akiwa chama cha Alianz katika mwaka wa 1997. Akawa makamu wa rais katika uchaguzi wa rais wa 1999 kwa Rais Fernando de la Rua, lakini alijiuzulu cheo chake tarehe 6 Oktoba 2000, [1] kutokana na makosa ya uchaguzi wa mawaziri. Yeye alistaafu kutoka maisha ya kujulikana na siasa kwa miaka mitano mpaka kuteuliwa kwa kazi ya Mercosur katika mwezi wa Desemba 2005.