Eduardo Duhalde

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wasifu
Rais wa 53 wa Argentina
2 Januari 2002 hadi 25 Mei 2005
Rais kabla yake: Eduardo Camaño
Rais baada yake: Néstor Kirchner
Naibu wa rais wa 30 wa Argentina
8 Julai 1989 – 10 Desemba 1991
Rais wake: Carlos Menem
Naibu kabla yake: Víctor Hipolito Martínez
Naibu baada yake: Carlos Ruckauf
Gavana wa Buenos Aires
10 Desemba 1991 – 10 Desemba 1999
Kabla yake: Antonio Cafiero
Baada yake: Carlos Ruckauf
Kibinafsi
Alizaliwa: 5 Oktoba 1941 (1941-10-05) (umri wa miaka 68)
Mahala pa kuzaliwa:Lomas de Zamora, Greater Buenos Aires
Uzalendo: Argentina
Chama : Chama cha Justicialista
Mke : Hilda de Duhalde
Kazi : Mwanasheria

Historia fupi[hariri | hariri chanzo]

Eduardo Alberto Duhalde [2] (alizaliwa 5 Oktoba 1941) ni rais wa zamani wa Argentina.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Duhalde alizaliwa Lomas de Zamora, katika eneo la Greater Buenos Aires. Yeye alifuzu kama mwanasheria katika mwaka wa 1970. Katika mwaka wa 1987, akawa mwanachama wa Argentina National Congress na akawa makamu wa rais chini ya Carlos Menem kuanzia mwaka wa 1989 hadi alipojiuzulu katika mwaka wa 1991. Katika mwaka wa 1991,alishinda muhula ya kwanza kama gavana wa Buenos Aires na akashinda muhula ya pili baadaye.

Aligombea kiti cha urais katika mwaka wa 1999, baada ya Carlos Menem kushindwa kushinda muhula ya tatu, lakini akashindwa na Fernando de la Rúa. Duhalde alichukua nafasi ya pili katika uchaguzi huo na asilimia 37 ya kura. Baada ya de la Rúa kujiuzulu kwa sababu ya shida za kiuchumi na maandamano ya Desemba 2001,Duhalde aliteuliwa kama Rais wa Argentina na Bunge mnamo 2 Januari,2002 baada ya mfululizo wa matukio ambayo watu wanashuku kuwa njumu.

Watu katika maandamano akaunti zao za benki zilipofungwa wakati nchi hiyo ilikuwa na shida za kiuchumi hapo mwaka wa 2002

Hapo awali,alifa kufanya kazi katika ofisi hiyo kwa miezi kadhaa hadi maandamano nchinin yaishe lakini Duhalde alibaki ofisi kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja. Wakati huo, yeye alithibitisha mingi ya deni la Argentina na akafanya uamuzi uliosababisha mfumuko wa bei, kutoridhika kwa raia na akaacha zaidi ya nusu ya Argentina wakiwa fukara. Licha ya hayo, alipewa sifa mbaya kwa kusema watu waliohifadhi madola watalipwa madola kabla ya kulazimisha kubadilishwa kwa dola na peso kwa bei ya peso 1.40 kwa dola moja,hii ilikandamiza watu. Duhalde aliweza kuimarisha vurugu katika uchumi na,chini ya shinikizo kutoka wanasiasa, akaagiza uchaguzi ufanyike miezi sita kabla ya tarehe iliyopangiwa.

Duhalde alifuatiwa na Néstor Kirchner mnamo 25 Mei 2003. Usaidizi wa kisiasa wa Duhalde kwake Kirchner dhidi ya Carlos Menem ulionekana kama mpango wa Duhalde kuendelea kuongoza kinyumanyuma. Baada ya muda mdogo, hata hivyo, Kirchner aliendelea kuachana na Duhalde. Mke wa Duhalde,Hilda Chiche Duhalde,aliendesha kampeni kali ya Seneti ya kuwakilisha Buenos Aires dhidi ya mke wa Kirchner, Cristina Kirchner, katika uchaguzi wa bunge wa 23 Oktoba 2003. González alishindwa kwa kura nyingi,kulingana na uchambuzi na wanasiasa huu ndio uliokuwa mwisho wa utawala wa Duhalde katika jimbo hilo.

Duhalde alithibitisha nia yake ya kugombea tena kiti cha urais mnamo tarehe 23 Desemba 2009. Alisema kuwa rais wa zamani Nestor Kirchner alikuwa amelevya na utawala.Atashindana na mgombeaji yeyote atakayesaidiwa na rais wa sasa Cristina Fernández de Kirchner na rais wa zamani Nestor Kirchner katika uchaguzi wa msingi katika Chama cha Justicialista.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]