Nenda kwa yaliyomo

Ukanoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Can.Reg.)
Askofu Mbenedikto Chrodegang wa Metz ni kati ya waliohamasisha Ukanoni katika karne ya 8.

Ukanoni ni mtindo wa maisha ya kitawa katika kanisa katoliki uliokusudiwa hasa kwa mapadri wa parokia za mjini.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Ili kuboresha maisha ya mapadri wanajimbo, toka zamani ulisisitizwa uundaji wa jumuia kati yao, ambamo wasali na kufanya utume kwa pamoja.

Hasa kuanzia karne XI wengi walifanya hivyo kwenye makanisa makubwa kama mtindo mpya wa kitawa unaosisitiza liturujia ya fahari pamoja na uchungaji.

Inavyoweza kueleweka, hao walifuata kanuni ya Agostino wa Hippo na kuitwa Wakanoni. Maarufu zaidi katika yao ni Norbert (1082-1134), mwanzilishi wa Wapremontree.

Leo mtindo huo unaendelea katika mashirika mbalimbali, ambayo lakini hayana watu wengi kama aina nyingine za utawa.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.