Nenda kwa yaliyomo

Myombo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Brachystegia)
Myombo
(Brachystegia spp.)
Myombo wa Boehm (B. boehmii)
Myombo wa Boehm (B. boehmii)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Planta (mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Fabales (Mimea kama mharagwe)
Familia: Fabaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mharagwe)
Nusufamilia: Caesalpinioideae
Jenasi: Brachystegia
Benth.

Miyombo ni aina za miti inayoitwa na wanabiolojia kwa jina Brachystegia. Jina la Kiswahili linatoka wingi wa jina la Kibemba: "muombo (miombo)", lakini kwa sababu fulani wingi huu umekuwa umoja kwa Kiswahili: "myombo (miyombo)".

Miti hii inaunda misitu isiyo minene hasa katika mazingira makavu kiasi ya Afrika ya Mashariki na Kusini hasa katika nchi Zimbabwe, Zambia, Msumbiji, Angola, Tanzania na Malawi. Misitu ya miyombo inafunika maeneo ya kilomita za mraba milioni 5.

Misitu ya miyombo humwaga majani wakati wa majira ya ukame kwa kusudi la kuhifadhi maji ndani yao. Kabla ya kuja kwa majira ya mvua huotesha majani mapya. Wakati wa mabadiliko haya majani yanaonyesha rangi za dhahabu na nyekundu zinazopendeza.

Miyombo inayopatikana mara nyingi ni hasa Brachystegia boehmii na B. longifolia.[1]

Miyombo na watu[hariri | hariri chanzo]

Misitu ya miyombo ni muhimu kwa maisha ya watu wanaoishi karibu nayo wakivuna hapa matunda, asali, kuni na lishe kwa mifugo. Kukatwa kwa miti hii imezidi kutokana na kuongezeka kwa watu na matumizi ya kuni. Utengenezaji wa makaa karibu na barabara kubwa yanayopelekwa mjini ni sababu muhimu. Katika maeneo ambako tumbako hulimwa wakulima wanakata miti mingi mno wakitumia kuni kukausha majani ya tumbako.

Wanyama[hariri | hariri chanzo]

Miyombo inaota kwenye ardhi isiyo na rutba sana. Hata hivyo misitu ya miyombo ni nyumbani kwa spishi nyingi za wanyama pamoja na ndege wanaoishi hapa pekee. Wanyamapori wengi wanapata kinga na lishe kati ya miti hii kama vile tembo, mbwa mwitu, na wengine.

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo na Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

  1. Smith, Paul & Allen, Quentin: Field Guide to the Trees and Shrubs of the Miombo Woodlands, Royal Botanic Gardens, Kew 2004.