Beseni kubwa la Marekani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Beseni Kubwa la Marekani.

Beseni Kubwa (Great Basin) ni eneo yabisi la Marekani kusini lililopo kati ya Sierra Nevada na Safu ya Wasatch. Ni mazingira makavu na sehemu zake zina tabia za jangwa, nyingine za mbuga kavu.

Tabianchi yake inaleta majira ya joto kali na kipindi cha baridi chenye theluji. [1] Sehemu kubwa ya beseni iko ndani ya jimbo la Nevada, ikigusa pia majimbo ya Utah, Kalifornia na Idaho. Eneo hili lina kilomita za mraba 541,730.

Sehemu hii inaitwa beseni kwa sababu inapokea maji -hata kama ni kidogo kutokana na joto- kutoka mvua mlimani lakini mito yake inaishia ndani ya beseni, hakuna njia ya maji kutoka na kuelekea baharini.

Eneo la Beseni Kubwa linafanywa na mabeseni madogo na mabonde 100 hivi, pamoja na milima kati yake. Uso wa ardhi ni hasa mbuga kavu, sehemu za jangwa, mabonde makavu ya mito ya awali na maziwa ya chumvi.

Mito ni michache, mikubwa zaidi ni mito ya Bear, Humboldt na Sevier ambayo yote inaishia katika mabeseni madogo ambako maziwa yanaweza kutokea katika miaka yenye usimbishaji mkubwa lakini hayadumu; ziwa kubwa zaidi ni Ziwa Kubwa la Chumvi karibu na Salt Lake City, Utah.

Kwa jumla maeneo ya Beseni Kubwa yana wakazi wachache; kuna maeneo ya miji mikubwa kando ya beseni lenyewe, moja ni eneo la Reno katika Nevada upande wa magharibi na Salt Lake City pamoja na miji jirani upande wa mashariki. Katikati kuna miji midogo tu.

Tabia za jangwa zinasababishwa na athira ya safu za milima zinazopakana na Beseni Kubwa na kumwaga kivuli cha mvua juu yake.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "What is the Great Basin?". National Park Service. Iliwekwa mnamo 2015-07-14. 
Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Beseni kubwa la Marekani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.