Aunt Ezekiel
| Aunt Ezekiel | |
|---|---|
| Amezaliwa | Gwantwa Ezekiel Grayson 28th October 1986 |
| Kazi yake | Mwigizaji, mtayarishaji wa filamu, |
| Miaka ya kazi | 2000-hadi sasa |
Gwantwa Ezekiel Grayson (Aunt Ezekiel) (alizaliwa Dar es Salaam, 28 Oktoba 1986) ni mwigizaji wa Tanzania aliyejulikana kwenye uigizaji wa filamu 'Prison Revenge’, ‘Pumba Jungu La Urithi’ na ‘Eyes on Me’.
Baba yake alijulikana kama Ezekiel Grayson ambaye alikuwa mchezaji bora wa timu ya mpira wa miguu Simba S.C..[1]
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Bunge mwaka 1993 hadi 1998. Alimaliza elimu yake ya msingi katika Shule ya Msingi Chanzige wilayani Kisarawe katika Mkoa wa Pwani.
Alianza Kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Kawawa na alifikia kidato cha pili, na kurudi Dar es Salaam na kumaliza kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Makongo.
Baada ya kumaliza Sekondari ya Makongo alijiunga na mafunzo ya Kompyuta Amana, na alishiriki mashindano ya urembo na kuibuka Miss Mwanza 2006.
Maisha ya ndoa
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 2007 alifunga ndoa ya bomani na mfanyabiashara Jack Pemba na kupata watoto watatu, ila baadaye akawa na mahusiano na dansa Mosse Iyobo na walizaa mtoto mmoja wa kike aitwaye Cookie. Kwa Sasa ana mahusiano na mwanamuziki aitwaye Kusah na wana Watoto wawili.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Aunt Ezekiel kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |