Ares, Promo na Elia
Mandhari
Ares, Promo na Elia (walifia dini Askalona, Palestina, 14 Desemba 308 au 309) walikuwa Wakristo wa Misri ambao waliuawa kwa imani yao wakielekea na wenzao wengi huko Kilikia kufariji waliopelekwa na kaisari Masimino Daia uhamishoni huko.
Walipofikia Kaisarea Baharini, walinyofolewa macho na kukatwa miguu kikatili, halafu wakapelekwa Askalona ambapo, kwa amri ya gavana Firmiliano, walikamilisha ushahidi wao, Ares kwa kuchomwa moto akiwa hai, wengine kwa kukatwa kichwa.[1]
Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 14 Desemba[2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |