Antoni wa Lerins

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Antoni wa Lerins (Hungaria, 468 hivi - Lerins, leo nchini Ufaransa, 520 hivi) alikuwa mmonaki maarufu kwa utakatifu na miujiza yake.

Baada ya kulelewa na Severino wa Noriko, alipofikia umri wa miaka 20 alijiunga na monasteri huko Ujerumani[1][2], halafu akawa mkaapweke katika Italia Kaskazini. Kwa kuwa alizidi kupata wafuasi na heshima, miaka miwili kabla hajafa alihamia Lerins ili kupata faragha aliyoitamani[3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 28 Desemba[4].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.