Ansgar Mtakatifu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mt. Ansgari akiwahubiri Waswidi.

Mtakatifu Ansgar (labda 8 Septemba 8013 Februari 865) alikuwa askofu mmisionari kutoka Ufaransa.

Tangu kale ametambuliwa kuwa mtakatifu.

Sikukuu yake ni 3 Februari[1].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Ansgar alizaliwa Amiens (Ufaransa) mwanzoni mwa karne ya 9.

Alisoma katika monasteri huko Corbie.

Mwaka 826 alienda kuhubiri Injili nchini Denmark, ambako hakufanikisha sana, hivyo akaenda Uswidi.

Aliteuliwa kuwa askofu wa Hamburg, upande wa kaskazini wa Ujerumani. Pia alikuwa balozi wa Papa Gregori IV katika Denmark na Uswidi.

Alivumilia magumu mengi sana katika kazi ya uenezaji Injili, lakini hakukata tamaa.

Alifariki huko Bremen (Ujerumani) mwaka 865.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Pryce, Mark. Literary Companion to the Festivals: A Poetic Gathering to Accompany Liturgical Celebrations of Commemorations and Festivals. Minneapolis: Fortress Press, 2003.
  • Tschan, Francis J. History of the Archbishops of Hamburg-Bremen. New York: Columbia University Press, 1959.
  • Wood, Ian. The Missionary Life: Saints and the Evangelisation of Europe, 400 – 1050. Great Britain: Longman, 2001.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.