Nenda kwa yaliyomo

Annobón

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Annobon)

Annobón (kwa Kihispania: Provincia de Annobón; [1] [2] kwa Kireno: Ano-Bom) ni kisiwa cha Guinea ya Ikweta kilichopo kwenye Ghuba ya Guinea ya Bahari Atlantiki upande wa kusini ya ikweta. Pamoja na visiwa vidogo vilivyopo karibu kinaunda mkoa wa Guinea ya Ikweta.

Kulingana na sensa ya 2015, Annobón ilikuwa na wakazi 5,314. Lugha rasmi ni Kihispania lakini wakazi wengi huzungumza lugha ya Krioli ya Kireno.

Sekta kuu za kiuchumi za kisiwa hicho ni uvuvi na misitu .

Mji mkuu wa mkoa ni San Antonio de Palé upande wa kaskazini wa kisiwa; mji mwingine ni Mabana, hapo awali ulijulikana kama San Pedro. Kuna nafasi salama ya kutua nanga na baadhi ya meli zinazopita huchukua fursa hiyo ili kupata maji na mahitaji mengine yanayopatikana Annobón.

Hata hivyo, hakuna ratiba za huduma ya usafirishaji kwa maeneo mengine ya Guinea ya Ikweta. Meli hufika mara kwa mara kama kila baada ya miezi michache.

Mahali pa Annobón katika Ghuba ya Guinea

Kisiwa cha Annobón ni volkano iliyozimika. Kisiwa kikuu kina ukubwa wa km 6.4 kwa urefu na km 3.2 kwa upana, na eneo la kilomita za mraba 17.

Ziwa lake la kati la volkeno linaitwa Lago A Pot na kilele chake cha juu zaidi ni Quioveo, ambacho kina urefu wa mita 698 juu ya UB.

Wakazi wa kisiwa hicho wana asili ya mchanganyiko wa Ureno na Angola, pamoja na mchanganyiko wa Wahispania. Wengi hawatumii Kihispania ambayo ni lugha rasmi ya nchi lakini aina ya Kireno.

Utamaduni unafanana sana na ule wa São Tomé. [3] Watu wengi ni Wakatoliki, ingawa kuna machanganyiko na dini za asili.[4]

  1. Ogunu, Oseni (2005). 1994-2003 (kwa Kiingereza). EMI. ISBN 978-88-307-1718-3.
  2. II censo de población y II de viviendas 1.994: Análisis demográfico. tema 01. Evaluación y ajuste de datos. tema 02. Estado de población. tema [03]. La fecundidad. tema 04. Análisis de la mortalidad. tema 05. Estudio de la migración. tema 06. Alfabetización, escolarización e instrucción. tema 07. Situación matrimonial y nupcialidad. tema 08. Caracteristicas económicas. tema 09. Análisis de las viviendas. tema 10. Hogares. tema 11. La mujer guineo-ecuatoriana. tema 12. Proyecciones demográficas (12 v.) (kwa Kihispania). La Oficina. 1997.
  3. "Ano Bom - A Ilha Esquecida no Meio do Atlântico". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2018-07-29.
  4. "Ilha de Ano-Bom estabelece ligação da Guiné Equatorial à lusofonia – DW – 05/08/2014". dw.com (kwa Kireno). Iliwekwa mnamo 2023-01-14.