Alipius wa Thagaste

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
"Wongofu wa Mt. Augustino" (mchoro wa Gozzoli). Huenda mtu aliye kulia kwake ni Alipius.[1]

Alipius wa Thagaste alikuwa askofu wa Tagaste (leo nchini Algeria) mwaka 394. Inasemekana ndiye wa kwanza kujenga monasteri sehemu hiyo ya Afrika.

Kwa muda mrefu sana alikuwa rafiki wa Augustino wa Hippo akaungana naye katika kuongokea Kanisa Katoliki (386; Confessions 8.12.28) na katika maisha ya kiroho.

Karibu yote tunayoyajua juu yake yanatokana na kitabu cha Augustino juu ya maisha yake mwenyewe Maungamo (Confessiones).

Papa Gregori XIII alimtangaza mtakatifu mwaka 1584[2] .

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Agosti[3][4].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Rotelle O.S.A., John. Book of Augustinian Saints (Augustinian Press, Villanova University, 2000)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.