Alibaba Group

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Makao makuu ya kampuni ya Alibaba Group huko Hangzhou

Alibaba Group Holding Limited (pia hujulikana kama Alibaba) ni kampuni ya teknolojia ya kimataifa yenye makao makuu yake nchini China iliyobobea katika biashara ya mtandaoni na teknolojia .

Ilianzishwa mnamo 28 Juni 1999 huko Hangzhou,Zhejiang kampuni hiyo hutoa huduma za mauzo ya watumiaji kwa watumiaji (C2C), biashara kwa watumiaji (B2C), na biashara kwa biashara (B2B) kupitia lango za wavuti, pia hutoa huduma za malipo ya kielektroniki, injini za utaftaji wa ununuzi, na huduma za kompyuta ya wingu. Inamiliki na kuendesha matawi mengi ya kampuni ulimwenguni kote katika sekta nyingi za biashara. [1]

Mnamo 19 Septemba 2014, uwekezaji wa shea wa Alibaba (IPO) kwenye Soko la hisa la New York ulikusanya dola za Kimarekani bilioni 25, na kuipa kampuni hiyo thamani ya soko la dola za Kimarekani bilioni 231. Hadi sasa IPO ni kubwa zaidi katika historia duniani.[2] Ni mojawapo ya mashirika 10 yenye thamani zaidi[3] na imetajwa kuwa kampuni ya 31 kwa ukubwa duniani kwenye orodha ya Forbes Global 2000 mwaka 2020.[4] Mnamo Januari 2018, Alibaba ilikuwa kampuni ya pili katika bara la Asia kwa kuwa na thamani ya dola Kimarekani bilioni 500, baada ya mshindani wake kampuni ya Tencent.[5]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alibaba Group kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.