Nenda kwa yaliyomo

Aleksandra wa Misri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Aleksandra wa Misri (aliishi katika karne ya 4) alikuwa mwanamke Mkristo wa Aleksandria ambaye tangu umri wa miaka 20 alijifungia kuishi katika aina ya kaburi lenye dirisha kwa ajili ya kupewa chakula. Aliishi hivyo miaka kumi hadi kifo chake.

Habari zake ziliandikwa na Palladi wa Eleonopolis na Melania Kijana.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Februari, siku aliyofariki[1].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]