Albert Liurette

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Albert Liurette (alizaliwa Kouta, Julai 3 1904 ila tarehe ya kifo chake haijulikani) alikuwa daktari na mwanasiasa kutoka nchini Guinea.

Liurette alisomea masomo ya udaktari katika chuo cha Ecole de medicine akapata astashahada ya tiba za Kiafrika.[1] Kabla ya mwaka 1951, katika uchaguzi wa wabunge wa Ufaransa mnamo Juni 17, 1951 kwenye Bunge la Kitaifa la Ufaransa, Liurette aliwekwa katika nafasi ya pili kwenye orodha ya Sehemu ya Ufaransa ya Wafanyakazi wa Kimataifa (SFIO). Alipata kura 67,480 sawa na (30.5%), SFIO ilishinda viti viwili kati ya vitatu vilivyopewa na Guinea. Yaciné Diallo na Liurette walichaguliwa kwa Bunge.[2]

Liurette alikuwa katibu wa Bunge la kitaifa mnamo Januari mwaka 1955.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Albert Liurette kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.