Nenda kwa yaliyomo

Abondi wa Como

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Abondi wa Como

Sura yake.
Feast

Abondi wa Como (Thesalonike, Ugiriki - Como, Lombardia, 468 BK[1]) anakumbukwa kama askofu wa 4 wa Como (Italia Kaskazini) kuanzia mwaka 448.

Askofu Amansi wa Como alimpa upadirisho akamfanya mwandamizi wake[2].

Papa Leo I alimtuma Konstantinopoli kutetea imani sahihi kuhusu Yesu Kristo dhidi ya Nestori na Eutike. Abondi alifanya hivyo kwa ari kubwa akishiriki mtaguso wa Konstantinopoli wa mwaka 448 halafu mtaguso wa Kalsedonia (451). Baadaye alishiriki pia mtaguso wa Milano wa mwaka 452.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Aprili[3].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Jones, Terry. "Abundius of Como". Patron Saints Index. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Februari 2007. Iliwekwa mnamo 4 Machi 2007.
  2. [http://www.santiebeati.it/dettaglio/34400
  3. Martyrologium Romanum
  • Siro Borrani, Il Ticino Sacro. Memorie religiose della Svizzera Italiana raccolte dal sacerdote Siro Borrani prevosto di Losone, Tip. e Libreria Cattolica di Giovanni Grassi, Lugano 1896, 531.
  • Adriano Caprioli, Antonio Rimoldi, Luciano Vaccaro (a cura di), Diocesi di Como, Editrice La Scuola, Brescia 1986, 25, 29, 34, 36, 45, 49, 53, 55, 72, 81, 93, 95, 111, 128, 154, 163, 164, 167, 169, 170, 172, 179, 226.
  • Luciano Vaccaro, Giuseppe Chiesi, Fabrizio Panzera, Terre del Ticino. Diocesi di Lugano, Editrice La Scuola, Brescia 2003, 128, 226, 228, 280, 285, 443.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.